Ujenzi wa magodauni ya sita umepiga hatua kubwa…

Maoni katika picha
Ujenzi wa magodauni ya sita yanayo jengwa katika mkoa wa Karbala barabara inayo elekea katika eneo la Jamaliyya umepiga hatua kubwa, sawa na miradi mingine ya ujenzi kama huo, ambapo tunatarajia siku za usoni kitakua kituo kamili cha viwanda kitakacho nufaisha Atabatu Abbasiyya na mkoa wa Karbala kwa ujumla, hili ndio lengo kubwa la kuanzisha ujenzi wa majengo ya aina mbalimbali na ukubwa tofauti, yanatofautiana ukubwa na yanaungana katika lengo.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ambao ndio wasimamizi wakuu wa mradi huu kuanzia usanifu hadi ujenzi, Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, akaongeza kua: mradi huu unajengwa katika kiwanja chenye ukubwa wa (2m64,750) na umegawika sehemu mbili:

Sehemu ya kwanza ni majengo ya ghorofa mbili, kila jengo linaukubwa wa (2m3,000), na sehemu ya pili ni magodauni yenye kukubwa wa (2m2,500) yamesanifiwa na kujengwa kwa mtindo wa kumbi za wazi, na sehemu zote zimewekwa mfumo wa zima moto na alam za tahadharisho, pia kuna mfumo maalumu wa kamera za ulinzi na kuna mtandao wa njia za ndani na njia za maji, pamoja na sehemu za vyoo na vyumba vya ofisi na mengineyo, pamoja na mfumo wa njia zinazo endana na matumizi ya majengo haya”.

Akabainisha kua: “Hakika kazi ya ujenzi inaendelea vizuri pamoja na tatizo la kiuchumi lililopo katika Atabatu Abbasiyya tukufu na uchache wa bajeti, juhudi kubwa inafanyika kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya muda ulio pangwa, mradi huu unatekelezwa na shirika la ujenzi la Liwaaul-Aalamiyya chini ya usimamizi wa kitengo cha uhandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, hakika shirika hili linatekeleza mradi kama ulivyo pangwa, wamesha fanyiwa uhakiki katika sehemu zilizo kamilika, zimejengwa kwa ubora mkubwa na viwango vilivyo pangwa, pamoja na kuhakikiwa vifaa vinavyo tumika katika ujenzi.

Kumbuka kua mradi huu ni miongoni mwa miradi iliyo buniwa na kufanywa na Atabatu Abbasiyya, inayo lenga kujiendeleza kiuchumi kupitia nyanja ya magodauni na viwanda.

Ni vizuri kukumbusha kua kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimesha fanya makumi ya miradi mikubwa na mamia ya miradi midogo na miradi ya kati, -ukiwemo mradi huu- ndani na nje ya Ataba, sehemu kubwa ya miradi hii, imefanya na mafundi wa Iraq kwa kushirikiana na kitengo tajwa hapo juu pamoja na mashirika ya kitaifa ya nje ya Ataba, na mara chache mno wameshirikiana na mashirika ya kigeni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: