Bango ya kuomboleza kifo cha Imamu Swadiq (a.s) lawekwa juu ya mlango wa Kibla wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na uwanja wa haramu tukufu wajaa huzuni…

Maoni katika picha
Kama sehemu ya kuhuisha na kukumbuka tukio la kuumiza -kifo cha Imamu Jafari Swadiq (a.s)- limewekwa bango kubwa juu ya mlango wa Kibla wa Abulfadhil Abbasi (a.s) lenye urefu wa (mt: 28) na upana wa (mt: 6) limedariziwa kwa uzi mweupe maneno yasemayo (Allahumma swalli alaa Ja’afari bun Muhammad Hujjatu Rabbul-Aalamiin) na pembezoni mwa uzi huo kumedariziwa maneno yasemayo (Swaadiqun fil-qauli) na (Swaadiqun fil-fi’li) kwa rangi ya kijani.

Kwa upande mwingine kuna bango lingine limewekwa juu ya mlango wa Imamu Hassan (a.s) unao elekea katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, lenye urefu wa (mt:16) na upana wa (mt:6) limedariziwa maneno yasemayo (Assalaamu alaika yaa Ja’faru bun Mauhammad Swaadiq) kwa langi ya kijani, na chini yake kuna maneno yasemayo (Yaa Swadiqan bilqauli walfi’ili) kwa rangi nyeupe.

Imetanda huzuni katika Atabatu Abbasiyya tukufu na katika korido zake zote za ndani na nje, kila sehemu imewekwa mapambo meusi kama alama ya huzuni, kwa ajili ya tukio hili linalo umiza la kuuawa kishahidi kwa Imamu Swadiq (a.s) lililo tokea tarehe ishirini na tano katika mwezi wa Shawwal, zimepandishwa bendera nyeusi na kuwashwa taa nyekundu kama ishara ya kuomboleza msiba huu na kumpa pole Mtume Mtukufu na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu kama kawaida yake kila mwaka, imeandaa ratiba kamili ya maombolezo ambayo imejumuisha vitu vingi, kama vile kutolewa mawaidha mbalimbali na kufanya majlisi maalumu za kuomboleza msiba huu, pia imejiandaa kupokea misafara (Mawakibu) ya waombolezaji wanaokuja kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: