Idhaa ya Alkafeel sauti ya mwanamke wa kiislamu yatangaza mashindano ya wahadhiri wa kike wa mimbari ya Husseiniyya…

Maoni katika picha
Idhaa ya Alkafeel sauti ya mwanamke wa kiislamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo ipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni imetangaza mashindano ya wahadhiri wa kike wa mimbari ya Husseiniyya, nayo itakuwa ni uwasilishaji wa maudhui zitakazo teuliwa chini ya kanuni za mashindano, washiriki wa mashindano watatumia kanuni za utowaji wa khutuba (muhadhara) kuanzia utangulizi, uwasilishaji na hitimisho na kitu chochote atakacho amua kuongeza muongeaji katika maudhui.

Masharti ya mashindano

 • 1- Mada: Iwe ya kijamii inayo husu wanawake (wanawake wa Ahlulbait (a.s) na wanawake wa Twafu watatumika kama mfano) chini ya kanuni zifuatazo:
 • A- Khutuba isizidi kurasa mbili (yasizidi maneno 540), ukubwa wa hati uwe saizi 16 aina ya hati iwe Times New Roman, hamishi (pembezoni mwa maandishi) iwe 0.5, aandike nukta muhimu za mada katika muhtasari mfupi unao eleweka.
 • B- Akabidhi khutuba yake ikiwa imerekodiwa kwenye CD.
 • C- Ajiepushe kutolea mifano watu binafsi au kuelemea mlengo fulani ispokua maeneo matukufu kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s).
 • D- Katika CD hiyo aelezee kwa ufupi historia ya maisha yake ya uhadhiri, namba ya simu, idadi ya miaka ambayo amekua akitoa mihadhara na majlis mashuhuri zaidi alizo wahi kuhutubia.
 • E- Mada yeyote ambayo haitakidhi vigezo tulivyo taja haitazingatiwa.
 • 2- Muda wa kuwasilisha khutuba ni dakika 5 hadi 15, maswali kuhusu mahadhi dakika 10.
 • 3- Kutuba na nai iandikwe kwa ufupi katika palagrafu moja.
 • 4- Mshiriki awe ni miongoni mwa wahadhiri wa mimbari ya Husseiniyya na awe na uzowefu wa mada anayo wasilisha, uchunge kanuni za uwasilishaji wa mada, kama hakupitia katika shule yeyote ya kufundisha namna ya kutoa khutuba basi awe na uzowefu usio pungua miaka 5.
 • Tarehe ya mwisho ya kupokea khutuba hizo itakua 29 Dhulqa’ada sawa na 12/08/2018.
 • Tarehe moja Dhulhijja khutuba hizo zitakabidhiwa kwenye kamati ya siri inayo undwa na wabobezi wa mimbari ya Husseiniyya chini ya Darul-khitwaaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu itakayo chagua khutuba 16 miongoni mwa khutuba zitakazo shiriki (kazi hiyo itakamilika mwezi 14 Dhulhijja).
 • Washindi wataitwa kwa mahojiano ndani ya studio ya idhaa ya Alkafeel katika mji mtukufu wa Karbala kuanzia mwezi 15 Dhulhijja sawa na 28/08/2018 hadi mwezi 29 Dhulhijja sawa na 10/09/2018 (kazi hiyo itachukua siku 15), watatoa khutuba na kusoma nai mbele ya majaji watatu 3 wabobezi wa fani zifuatazo:
 • 1- Ustadhat mbobezi wa Nahau na fani za lugha ya kiarabu.
 • 2- Ustadhat mbomezi wa mahadhi ya uongeaji.
 • 3- Ustadhat mbobezi wa utowaji wa khutuba.

Zawadi za washindi

 • 1- Zawadi ya mshindi wa kwanza: Atapewa nafasi ya kua mkufunzi katika Darul-khitwaaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
 • 2- Pia mshindi wa kwanza atapelekwa kumzuru bibi Zainabu (a.s).
 • 3- Mshindi wa pili atapewa laki moja na elfu hamsini (150,000) dinari za Iraq.
 • 4- Mshindi wa tatu atapewa elfu sabini na tano (75,000) dinari za Iraq.

Khutuba peke yake ndiyo itakayo rushwa kwenye redio bila nai kwa ajili ya kufuata sheria, na khutuba hizo zitarushwa katika siku za mwezi wa Muharam na zitawekewa sehemu ya kupiga kura kwa kila khutuba, ili kuitambua khutuba itakayo sikilizwa zaidi na itakayo athiri zaidi, wasikilizaji wataweza kuweka alama ya (pendeza), kura zitaanza kupigwa mwanzoni mwa mwezi wa Safar hadi mwezi 23, kura hizo zitaingizwa katika alama walizo pata kutoka kwa kamati ya majaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: