Muhimu… Marjaa dini mkuu abainisha msimamo wake kuhusu maandamano yanayo endelea katika mkoa wa Basra ya kupinga upungufu mkubwa wa huduma za kijamii…

Maoni katika picha
Marjaa dini mkuu amebainisha msimamo wake kuhusu maandamano yanayo shuhudiwa katika mkoa wa Basra kulalamikia ubovu wa huduma za kijamii, katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa ya leo ndani ya ukumbi wa haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, ifuatayo ni nakala ya khutuba hiyo:

Mabwana na mabibi! Katika siku hizi tunashuhudia maandamano ya amani katika mkoa kipenzi wa Basra na miji mingine, wananchi wanatoa madai mbalimbali kuhusu upungufu mkubwa wa huduma za kijamii, kama vite umeme pamoja na ongezeko la joto, upungufu mkubwa wa maji safi ya kunywa pamoja na mahitaji mengine muhimu ya kibinadamu, sambamba na ukosefu wa ajira na uchumi mbaya na upungufu wa vituo vya afya pamoja na kuwepo kwa ongezeko kubwa la maradhi katika mkoa huo.

Hatuna la kufanya zaidi ya kuungana na ndugu zetu wapenzi katika kudai haki, tunahisi uchungu mkubwa walio nao, na hali ngumu ya maisha wanayo pitia, hakika kuna uzembe wa wazi uliofanywa na viongizi wa zamani na wasasa wa kuboresha mazingira ya utowaji wa huduma za kijamii, pamoja na kuwepo uwezekano wa kifedha, kama wangetumia vizuri fedha na wakawatumia wataalamu na kusimamia vizuri utendaji wa ofisi za serikali, na kuwapiga vita mafisadi bila kujali chama au kundi fulani hali isingekua mbaya kama ilivyo leo.

Hakika mkoa wa Basra ni wakwanza katika kuchangia pato la taifa, pia ni mkoa wa kwanza kwa kuwa na mashahidi wengi pamoja na majeruhi katika vita ya kulikomboa taifa dhidi ya magaidi wa Daesh, barabara zao zimejaa picha za maelfu ya mashahidi walio jitolea roha zao kwa ajili ya kuikomboa Iraq na kulinda raia wake na maeneo matukufu, sio haki na wala haikubaliki mkoa huu kuwa wenye hali ngumu na kukosa huduma muhimu za kibinadamu, asilimia kubwa ya wakazi wa mkoa huo wanamaisha magumu, na mkoa unaupungufu mkubwa sana wa huduma za kijamii, pia kuna mripuko wa mafadhi kutokana na ubaya wa mazingira, asilimia kubwa ya vijana hawana kazi za kuwawezesha kujikimu kimaisha.

Viongozi wa serikali ya mkoa na serikali kuu wanatakiwa kuyafanyia kazi madai ya raia haraka iwezekanavyo na utendaji uanze mara moja katika mambo yanayo weza kuanza kutekelezwa, na kuweka utaratibu wa wazi na unao eleweka wa kutatua matatizo mengine yanayo lalamikiwa, sambamba na kuwa na msimamo mkali wa kisiasa unao piga vita mafisadi na kuwazuia kutumia mali za taifa kwa manufaa yao binafsi, hali kadhalika wawatumie wataalamu wenye uwezo na wasio kuwa na kashfa za kula mali za umma ili kupata ufumbuzi wa kweli katika tatizo hili, na sio kutupia watu wengine lawama na kuwabebesha mzigo wa yaliyo tokea na yanaendelea kutokea kwa wakazi wa mkoa huo kipenzi, wakazi wa mkoa huo wamekua wakidai haki zao kwa nyakati tofauti bila mafanikio na zaidi hali ilizidi kua mbaya.

Tunatarajia waandamanaji wasitoe usumbufu wowote kwa raia, na wala wasifanye mambo yasiyo faa katika kuonyesha hasira zao, wala wasimruhusu mtu yeyote kufanya uharibifu katika mali za serikali au za watu binafsi au za kampuni, ukizingatia kua uharibifu wowote utakao fanyika utafidiwa kwa mali za raia mwenyewe.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: