Kituo cha elimu na kukuza vipaji Alkafeel chaendesha nadwa ya kuitambulisha App ya Siraaj mtandao wa kishule…

Maoni katika picha
Mbele ya kiongozi mkuu wa kisheria wa Akatabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na idadi kubwa ya viongozi wa idara mbalimbali na wakuu wa vitengo, kituo cha elimu na kukuza vipaji ambacho kipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya kinaendesha nadwa ya kuitambulisha App mpya iitwayo Siraaj, ambayo inawaunganisha viongozi wa shule na wazazi/walezi wa wanafunzi, na inasaidia kuunganisha juhudi za mwalimu na mzazi katika kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi, itasaidia sana sekta ya elimu na malezi hapa Iraq.

Wahudhuriaji walisikiliza kwa makini maelezo yaliyo ambatana na picha za video katika kusherehesha vipengele muhimu vilivyopo katika App hiyo na namna ya kuitumia, pamoja na kufafanua milango iliyomo katika App na faida zinazo weza kupatikana kutokana na matumizi yake sambamba na kutoa mifano hai ya mafanikio ambayo yamesha patikana katika shule kadhaa kutokana na kutumia kwao App hiyo.

Kisha wahudhuriaji waliuliza maswali na kutoa maoni yao kuhusu App hiyo, na jopo la watalamu lilijibu maswali na kutoa ufafanuzi zaidi pale ilipo hitajika, ukizingatia ubora wa App hii na urahisi wa kuipakua.

Kiongozi wa kituo Ustadh Saamir Falaah Hassan Swafi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “App ya Siraaj imeleta maendeleo mazuri katika sekta ya malezi na elimu, imesanifiwa na kutengenezwa baada ya uchunguzi wa kina pamoja na kushauriana na watafiti walio bobea katika sekta ya elimu, ili kuhakikisha tunafungua App bora zaidi katika sekta hii, yenye mpangilio mzuri.

Akabainisha kua: “Hakika App hii imesha tangazwa rasmi katika baadhi ya maeneo baada ya kuonyesha mafanikio katika majaribio yaliyo fanyika kwenye shule zaidi ya moja, kote ilionyesha mafanikio makubwa kwa kurahisisha ushirikiano baina ya wazazi na viongozi wa shule, tunatoa wito kwa shule zote za msingi na sekondari (upili) zitumie App hii, itawaondolea vikwazo vya mawasiliano, na itachangia kuboresha maendeleo ya mwanafunzi kimasomo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: