Kamati ya majaji wa mashindano Karbala ya waimbaji wa mimbari za Husseiniyya yatangaza majina ya washindi…

Maoni katika picha
Kamati ya majaji wa mashindano ya Karbala ya waimbaji wa mimbari za Husseiniyya yatangaza majina ya washindi katika hafla ya kufunga mashindano iliyo fanyika jioni ya leo Juma Tano (18/07/2018m) sawa na (3 Dhulqa’ada 1439h) katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, matokea ya kikundi cha wanao chipukia ni kama yafuatavyo:

Mshindi wa kwanza: Mwimbaji Ridha Athiir Adnaan.

Mshindi wa pili: Mwimbaji Haidari Ali Nasoro.

Mshindi wa tatu: Mwimbaji Ali Hussein Haadi.

Kitengo cha habari na utamaduni kimeongeza zawadi ya mshindi wa nne na wa tano kwa ajili ya kutia hamasa zaidi kwa washiriki, zawadi hizo zilikabidhiwa na makamo raisi wa kitengo hicho, Sayyid Aqiil Yasiri na zilienda kwa:

Mshindi wa nne: Mwimbaji Muammal Ahmadi Mirza.

Mshindi wa tano: Mwimbaji Abbasi Muhsin Ali.

Matokeo ya kikundi cha vijana yalikua kama yafuatavyo:

Mshindi wa kwanza: Mwimbaji Amiir Ahmadi Azizi.

Mshindi wa pili: Mwimbaji Mustafa Risaan Alwaan.

Mshindi wa tatu: Mwimbaji Amiir Ali Adnaan.

Kamati ya majaji imesema kua; washiriki wote wamefanya vizuri, kila mmoja alikua na kitu cha tofauti na wenzake, tofauti zao ni ndogo ndogo sana, baadhi yao wametofautiana kwa nusu hadi robo ya alama ambazo zimetumiwa na kamati ya majaji kugawa matokeo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: