Wawakilishi wa kitengo cha mawakibu wa mikoani: Uhuishaji wa maadhimisho ya Husseiniyya unatakiwa ufuate misingi ya dini na kusahihisha vitendo visivyo faa vinavyo weza kufanywa na wajinga au wanafiki…

Maoni katika picha
Wawakilishi wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya wamesisitiza kua: Hakika maadhimisho ya Husseiniyya ni miongoni mwa turathi muhimu ya kidini na kitamaduni, ufanyaji wa maadhimisho hayo lazima uzingatie misingi ya dini na kusahihisha vitengo visivyo faa vinavyo weza kufanywa na wajinga au wanafiki.

Hayo yamesemwa katika hafla ya kuadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa kwa kitengo hicho, iliyo fanyika leo Juma Mosi (7 Dhulqa’ada 1439h) sawa na (21 Julai 2018m) katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, katika ujumbe ulio wasilishwa na bwana Saadi Abdali ambaye ni kiongozi wa wawakilishi wa mkoa wa Diwaniyya.

Aliongeza kusema kua: “Hakika huu ni urithi wa kidini na kitamaduni, hakika umma uliotengenezwa na Mtume (s.a.w.w) na ukakubali mafundisho yake, ukaangaziwa nuru yake hauwezi kufa, utaendelea kua tishio kwa madhalimu na magaidi, kulikua na umuhimu wa kuunda chombo cha Husseiniyya kitakacho ratibu na kusimamia shughuli za maadhimisho ya Husseiniyya, kwa sababu kitu chochote kinacho fanyika bila mpangilio huharibika na hakidhibitiki, kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kinafanya kazi kubwa ya kuandaa, kupangilia na kusajili mawakibu Husseiniyya katika mikoa yote ya Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu na hili ndio jukumu kubwa la kuanzishwa kwa chombo hiki”.

Akaongeza kua: “Baada ya kuanzishwa mawakibu Husseiniyya zenye jukumu la kutoa huduma, zimefanya kazi kubwa, zimetoa huduma hadi ya kupokea wakimbizi na kuwapa sehemu za kuishi pamoja na kuwapa kila kitu cha lazima katika maisha ya mwanadamu, wameitikia wito wa Marjaa dini mkuu wa jihadi ya kifaya, wakaingia katika uwanja wa kujitolea kwa kushika siraha na kuingia vitani au kutoa misaada ya kibinadamu kwa wapiganaji”.

Akaendelea kusema kua: “Kutokana na uzowefu wetu na utendaji wa wawakilishi wetu, tunawataka muendelee hivyo hivyo kuyafanyia kazi maelekezo yote yanayo tolewa na Marjaa dini mkuu pamoja na viongozi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), na kuhakikisha kitengo kinapanua utendaji wake katika nchi zote, na kupiga vita mitazamo isiyo faa katika maadhimisho ya Husseiniyya, na kunufaika na mwenendo wa Imamu Hussein (a.s) pamoja na tabia zake”.

Akasisitiza kua: “Tumekua tukishirikiana vizuri na vyombo vya serikali katika misingi ya kushauriana na kutegemeana”.

Akabainisha kua: “Tumetoa mashahidi kwa ajili ya kuilinda Iraq na maeneo matukufu na maadhimisho ya Husseiniyya tukiitikia wito wa Marjaa dini mkuu, tuna ahidi upya kua tutaendelea kufuata maelekezo ya Marjaiyya na kutembea chini ya nuru zao, tusimame kuonyesha heshima kwa mashahidi wa Iraq na mashahidi wa mimbari ya Husseiniyya walio jitolea nafsi zao kwa ajili ya kuitikia wito wa Marjaa dini mkuu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: