Kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati chatoa wito kwa watafiti wa kushiriki katika mradi uitwao (Magharibi katika kioo cha safari za waislamu)…

Maoni katika picha
Kituo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya kimetoa wito kwa watafiti wajitokeze kushiriki katika mradi uitwao (Magharibi katika kioo cha safari za waislamu), ambao ni mradi wa kufanya utafiti kwa vikundi wa kuangalia safari hizo na kufanya uchambuzi wa kina, kufanya hivyo inawasaidia watafiti (kutambua mambo ya ajabu) na kufahamu namna ya kuwasilisha ujumbe wa kiislamu katika jamii za watu wa Magharibi, pia kufahamu nukta imara na dhaifu, pamoja na kufahamu hatua walizo tumia katika jamii za kiislamu baada ya kurudi kwao, je, hatua hizo zilizo chukuliwa na watu wa Magharibi zimeingiza tamaduni za kimagharibi katika jamii za kiislamu na kuondoa sura ya kiislamu, au zimechangia katika kuendeleza hali za waislamu.

Kituo kimetoa masharti ya ushiriki kama ifuatavyo:

  • 1- Lazima uzungumzie safari zilizo nakiliwa, zilizo fanyika kabla ya zama za maendeleo au baada yake.
  • 2- Kuwasiliana na idara ya wahariri kwa ajili ya kujisajili na kuchagua mada.
  • 3- Kutotosheka na ya kusifu bali ulazima wa kuandika na maelezo ya ukosowaji.
  • 4- Ukurasa mmoja uelezee wasifu wa muandishi mhusika wa safari.
  • 5- Utafiti usiwe zaidi ya kurasa (25).
  • 6- Utafiti utakua mali ya kituo na kitakua na haki ya kuurudufu na kuutafsiri katika lugha zingine.
  • 7- Zitatolewa zawadi za pesa kwa watafiti.
  • 8- Muda wa juu wa kutuma tafiti ni miezi (4).
  • 9- Kufanyia kazi maono ya kamati ya watalamu kama yakipatikana.
  • 10- Kuwasiliana na ofisi inayo simamia mradi huu na tafiti zitumwe kupitia barua pepe ifuatayo: css.ib@gmail.com

Kumbuka kua safari za Magharibi ni miongoni mwa sababu kubwa za waislamu kuitambua Magharibi moja kwa moja, waliandika waliyo yashuhudia na wakaelezea safari zao kwa urefu kiasi mwanafunzi wa Magharibi hawezi kuelewa mambo yote, kuna vitabu vingi sana katika ulimwengu wa kiislamu vinavyo elezea safari hizo za Mashariki na Magharibi, na vinaendelea kusambaa hadi leo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: