Katika juhudi zake za kuhakikisha kinatoa elimu ya sekula: Chuo kikuu cha kimataifa Al-Ameed chaingizwa katika orodha ya (Webometrics)…

Maoni katika picha
Matokeo ya hivi karibuni ya taasisi ya kimataifa ya (Webometrics) inayo pima ubora wa vyuo vikuu vya serikali na binafsi ya nchini Hispania, ambayo ni taasisi kubwa kimataifa inayo simamia ubora wa vyuo vikuu vya kimataifa zaidi ya (20,000), imetangaza jumla ya vyuo vikuu (16,000) hivi karibuni, kikiwemo chuo cha Al-Ameed ambacho kipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kua miongoni mwa vyuo bora sambamba na vyuo vikuu vingine vya serikali ya Iraq.

Makamo rais wa chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Muayyad Amraan Alghazali amesema kua: “Hakika kuingizwa kwa chuo kikuu cha Al-Ameed katika orodha ya vyuo vikuu bora kimataifa kunatokana na juhudi za kutoa elimu bora ya sekula miongoni mwa vyuo vikuu vya Iraq na kuchuana na vyuo vingine vya kimataifa kiasi chuo kimeweza kufikia vigezo vya kimataifa, hii ni ishara nzuri ya kuendelea kwa elimu hapa Iraq, kunatoa matumaini ya kuendana na maendeleo ya vyuo vikuu vya kisasa duiniani”.

Akasisitiza kua: “Hii ni miongoni mwa orodha muhimu za vyuo vya kisekula ambayo vyuo vingi hufanya juhudi ya kuingizwa katika orodha hiyo; kwani orodha hiyo huangalia ubora wa elimu inayo tolewa na chuo pamoja na maendeleo ya chuo kwa ujumla, pia vyuo vinavyo ingizwa katika orodha hiyo hutakiwa kutoa mikakati yao ya elimu na viwango vya elimu wanayo fundisha na hutangazwa katika mitandao maalumu ya intanet, hua ndio kipimo kikubwa cha kupata vyuo vyenye maendeleo katika orodha hiyo”.

Akaongeza kua: “Hakika tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha vituo vyote vinakua na maendeleo mazuri katika orodha hiyo, kupitia harakati tofauti za vitivo vya chuo hiki kwa kuhakikisha vinatoa elimu bora zaidi yenye viwango vya kimataifa, pamoja na mtandao wake wa kielektronik ambao ni miongoni mwa vipimo pia kwa kuangalia (uathiri, ufunguaji, kuingia na kupendezwa), ambao utatuwezesha kuendelea kubaki katika orodha hiyo”.

Kumbuka kua chuo kikuu cha Al-Ameed (kipo Karbala katika barabara ya Najafu – Karbala mkabala na nguzo namba 1238), nacho ni miongoni mwa taasisi muhimu za elimu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kilifungua kitivo cha kwanza cha udaktari katika ubora wa vyuo binafsi vya udaktari, na kinafuata mfumo wa elimu wa kimataifa, kwa ajili ya kuhakikisha kinafikia uwezo wa kutoa elimu bora zaidi, hukaribisha wabobezi mbalimbali katika fani tofauti, kwa ajili ya kunufaika na uzowefu wao na kupata ushauri wao kuhusu harakati za kielimu zitakazo kiwezesha chuo kua cha kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: