Kitengo cha malezi na elimu ya juu chaendesha semina ya kuwajengea uwezo watumishi wake zaidi ya (400) wakike na wakiume…

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinatoa mafunzo ya kijenga uwezo kwa washiriki zaidi ya (400), walimu na viongozi wa idara za elimu na malezi za shule za Ameed, kwa ajili ya kuongeza ujuzi na uwezo wao wa kufanya kazi, ili waendane na maendeleo ya ulimwengu wa sasa katika kila sekta.

Rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Abbasi Rashidi Didah ametuambia kua: “Program hii ni semina za kielimu, kimalezi na kiidara, yameandaliwa masomo maalumu na wakuu wa vitengo na wakufunzi wao katika idara ya elimu endelevu, walengwa wakuu katika semina hizi ni watumishi wa idara za elimu na malezi, program hii ni sehemu ya mazoweya yaliyopo katika ketengo hiki, ya kunufaika na ilicho nacho kwanza (watalamu wake), jambo hili lilitoa faida kubwa miaka ya nyuma kwa kuongeza uwezo wa walimu na watumishi wetu”.

Akabainisha kua: “Hakika semina hizi hutusaidia kufahamu uwezo halisi wa mwalimu, na kumfanya aendelee kutunza uwezo wake na kumsaidia kujiendeleza, kwani tuna amini kua semina ni mahala salama na panapo muendeleza mtu, wanasemina wanatoka katika idara za shule za Ameed kuanzia shule za chekechea na kuendelea, kwa ajili ya kuongeza uwezo wao na kuwashajihisha wenzao kuja kushiriki mwakani kutokana na mazuri waliyo yaona”.

Kiongozi wa idara ya elimu endelevu Dokta Muhammad Hassan Jaabir amefafanua kua: “Semina hizi, zinakusudia mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo: Zinaelekeza utendaji wa walimu wa shule za Ameed katika sekta mbalimbali, sekta ta elimu: kwa kufanya warsha za ufundishaji na uandaaji wa somo, na inahusisha kipengele cha mitihani ya majaribio, pamoja na kufafanua sifa za mwalimu mwenye mafanikio, sekta za malezi bora, vipaji vya akili, na vinginevyo”.

Kumbuka kua shule za Ameed ni sehemu ya taasisi za elimu na malezi zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ambapo kuna shule za msingi na sekondari (upili) pamoja na shule za awali (chekechea), shule hizi zina ufaulu mzuri kutokana na mikakati mizuri ya kielimu na kimalezi waliyo nayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: