Wasomaji wa Qur’an kutoka katika Maahadi ya Qur’an tawi la wasichana wamepata zawadi mbili katika mashindano mawili…

Maoni katika picha
Wasomaji wa Qur’an kutoka katika Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la wasichana chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu wamepata zawadi mbili, katika ushiriki wao wa mashindano mawili ya Qur’an, bibi Khalud Baaqir Abdul-Amiir alikua mshindi wa pili katika mashindano ya kuhifadhi juzuu (20) yaliyo kua na washindani (32), ambayo ni mashindano ya kitaifa yaliyo andaliwa na ofisi ya ufundishaji wa Qur’an chini ya idara ya tablighi tawi la wanawake katika Atabatu Husseiniyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Qur’an ndio njia ya ushindi wetu).

Mashindano ya pili yaliandaliwa na kituo cha Abu Hanifa Nu’maan kwa kushirikiana na kituo cha Iraq cha usomaji wa Qur’an tukufu, ambapo bibi Ruqayya Audah Abduzahra alikua mshindi wa kwanza katika mashindano ya kuhifadhi juzuu tano za Qur’an tukufu.

Kwa mujibu wa wasimamizi wa Maahadi ya Qur’an tawi la wasichana katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ushindi huu haujapatikana bure, unatokana na juhudi kubwa zinazo fanywa wakati wote na viongozi wa tawi chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, iliyo andaa mazingira bora yanayo wawezesha wasichana kuhifadhi Qur’an tukufu, ushindi huu ni dalili ya wazi ya ubora wa mfumo unao tumika.

Kumbuka kua hii sio mara ya kwanza ambayo wasomaji wa Qur’an kutoka katika Maahadi tawi la wasichana kupata ushindi, waliwahi kushiriki katika mashindano mengine siku za nyuma ambayo walipata ushindi pia, hii inaonyesha ubora wa mfumo unao tumiwa na Maahadi pamoja na idara yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: