Kwa ajili ya kuchangia kujenga jamii imara yenye mshikamano hususan jamii ya mayatima, kitengo cha malezi na elimu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya semina kwa mwaka wa pili mfululizo, ambayo imeanza jana siku ya Juma Tano, (18 Dhulqa’ada 1439h) sawa na (1 Agosti 2018m) yenye washiriki (97) wavulana na wasichana, semina hii inafanyika kwa watu wenye umuhimu zaidi wa kusaidiwa katika jamii.
Semina hiyo inaendeshwa ndani ya kumbi za shule za msingi za Ameed, kwa kipindi cha mwezi mzima, saa nne za masomo kwa kila siku, wanasomeshwa masomo yote yaliyopo katika selebasi, pia wana nyakati za mapumziko na mihadhara elekezi ya kidini, ili kuhakikisha wananufaika zaidi, wakufunzi wa semina hii ni watalamu kutoka katika kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
Jambo zuri katika semina hii, ni kuwashirikisha washiriki katika kusoma mada zilizopo mbele yao, jambo hilo linasaidia kujua mapungufu yao na sehemu ambazo hawazujui vizuri, kwa hiyo mwalimu anajikita katika kufundisha sehemu hizo na kuwafanya wazijue vizuri ili waweze kufaulu vizuri mtihani ujao, pia wanafunzi walio faulu wataandaliwa kwa ajili ya masomo ya mwaka ujao, fahamu kua masomo yeto yanafundishwa na walimu wenye utalamu mkubwa na kwa kufuata selebasi ya wizara ya malezi ya Iraq.
Kumbuka kua ushereheshaji wa masomo yote, katika semina hii unafanywa kisasa na kwa kutumia vifaa bora kabisa na vya kisasa, kwa ajili ya kufikisha fikra kwa njia bora zaidi kwa wanasemina.