Kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu chafunga taa za mapambo katika barabara ya Imamu Swahibu Zamaan (a.s)…

Maoni katika picha
Miongoni mwa barabara zilizo karibu na haram mbili tukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) ni barabara ya Swahibu Zamaan (a.f), ambayo ni miongoni mwa barabara za kibiashara za tangu zamani inayo tegemewa na mazuwaru wengi kufanya manunuzi yao wanao toka ndani na nje ya Iraq, pia ni barabara inayo ungana na mitaa mingi ya zamani inayo tokea katika barabara mbili muhimu, hivyo hapo ni sehemu muhimu, na hicho ndio kilicho pelekea kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu chini ya Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya kupitia idara ya umeme kuipamba barabara hiyo kwa kuweka taa nzuri za mapambo ambazo zimependezesha eneo hili tukufu.

Kuhusiana na jambo hili msimamizi wa kazi hiyo Muhandisi Thaair Adhaar Hashim amesema kua: “Idara ya umeme chini ya kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu imekamilisha kazi ya kuweka taa za mapambo katika barabara ya Swahibu Zamaan (a.s) kwa mafanikio makubwa, hakika taa za mapambo zilizo wekwa katika barabara hiyo zimechangia kwa kiasi kikubwa kupendezesha eneo hilo tukufu, ukiongeza na umuhimu wa barabara hii kwani ipo ubavuni mwa eneo la katikati ya haram mbili tukufu, na ina soko kubwa la kihistoria linalo tegemewa na idadi kubwa ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq, mafanikio haya makubwa ni sehemu ya mfululizo wa kazi nzuri za mafanikio zinazo fanywa na mafundi wa idara ya umeme”.

Akaongeza kua: “Tumetumia taa zenye rangi na maumbo mazuri zinazo tumia umeme kidogo, kazi hii imehusisha kuandaliwa kwa sehemu za kuweka nguzo za taa na uwekaji wa nguzo hizo kisha ufungaji wa taa na kuziunganisha na umeme”.

Kumbuka kua idara ya umeme ya kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu hubeba majukumu kadhaa, kama vile ufungaji wa nyaya za umeme, uwekaji wa taa, kusimamia mabango ya vituo vya ukaguzi na kuweka mapambo, pamoja na kazi zote zinazo husu umeme katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu na maeneo ya pembezoni mwake, pamoja na kazi endelevu za marekebisho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: