Idara ya shule za dini za Alkafeel yaandaa mashindano ya tafiti ya wanawake kuhusu bibi Zaharaa (a.s) na yatoa wito wa ushiriki wa watafiti wa kike…

Maoni katika picha
Idara ya shule za Alkafeel za wasichana chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa shindano la kitafiti kwa wanawake, shindano hilo litakua miongoni mwa ratiba (program) za kongamano la kitamaduni na kimataifa la Ruhu Nubuwwah awamu ya tatu, litakalo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Ewe Zaharaa ni wito wa kujitolea kwa ajili ya kuipamba mbingu), kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s), shindano hilo litahusisha mada zifuatazo:

  • 1- Haki za mke na utekelezaji wake katika sheria ya kiislamu kupitia maisha ya Swidiqah Fatuma Zaharaa (a.s).
  • 2- Kufanyia kazi uwelewa wa kiigizo chema kwa wasichana kwa ajili ya kuondoa matatizo ya vizazi, bibi Fatuma Zaharaa (a.s) kama mfano.
  • 3- Nafasi ya kinafsi na kidini katika historia ya Swidiqa Fatuma Zaharaa (a.s) katika zama za kudhihiri (dhuhuur).
  • 4- Kutawasal katika Maqaamu ya Swadiqah Fatuma Zaharaa (a.s) na kutafuta shifaa katika madhehebu za kiislamu.
  • 5- Elimu ya bibi Zaharaa (a.s) baina ya mji wa elimu na mlango wa elimu na kuakisi kwake kwa Maimamu Maasumina (a.s).
  • 6- Bibi Zaharaa (a.s) baina ya adabu mbili ya kiarabu na kifarsi.
  • 7- Malezi ya familia na misingi ya kinafsi, uchambuzi kutoka katika Qur’an tukufu na sunna takatifu (bibi Zaharaa “a.s” kama mfano).
  • 8- Dua za bibi Zaharaa (a.s) na tasbihi yake, (somo la kiitikadi – kiakhlaqi).
  • 9- Ufasaha wa wanawake wa nchi za uwarabuni katika zama za Utume, Swaidiqah Fatuma Zaharaa (a.s) kama mfano.

Mashariti ya mashindano ni:

  • 1- Utafiti usiwe umesha wahi kuandikwa au kusambazwa.
  • 2- Mada isewe kichwa cha utafiti.
  • 3- Utafiti usipungue kurasa (12) na usizidi kurasa (30) hati iwe na ukubwa wa saizi (16) na pembezoni mwa maandishi (hamishi) kuwe na ukubwa wa saizi (14) aina ya hati iwe ni (simplified Arabic).
  • 4- Pamoja na nakala ya karatasi aambatanishe na (cd) yenye jina la mtafiti, namba ya simu, barua pepe pamoja na wasifu wake (cv), utafiti ambao hautazingatia haya hautafanyiwa kazi.
  • 5- Pamoja na nakala ya utafiti, uambatanishwe na muhtasari wake usio zidi maneno (300).
  • 6- Mwisho wa kupokea tafiti hizo ni (mwezi mosi Rabiu Thani).
  • 7- Aandike marejeo na mapokeo yote kwa namba kwenye karatasi za mwishoni mwa utafiti.
  • 8- Utafiti hautarudishwa kwa aliye andika uwe umekubaliwa au haujakubaliwa.
  • 9- Hautakubaliwa utafiti wowote ambao hautaendana na mada tulizo taja.
  • 10- Matokeo ya utafiti yatatangazwa katika mtandao wa kimataifa Alkafeel.
  • 11- Wale ambao tafiti zao zitakubaliwa watapewa vyeti vya ushiriki, na kuna zawadi za washindi watatu wa mwanzo kama ifuatavyo:

Mshindi wa kwanza: (1,500,000) milioni moja na laki tano dinari za Iraq.

Mshindi wa pili: (1,250,000) milioni mojo laki mbili na elfu hamsini dinari za Iraq.

Mshindi wa tatu: 1,000,000) milioni moja dinari za Iraq.

Kumbuka kua malengo ya shindano hili ni:

  • - Kubainisha nafasi ya bibi Zaharaa (a.s) na utukufu wake katika sekta tofauti za uhai.
  • - Kufichua turathi za Mbora wa wanawake wa ulimwenguni na nafasi yake kifikra.
  • - Kushajihisha watafiti kuangazia sekta tofauti za matukufu ya bibi Zaharaa (a.s).
  • - Kuangalia mifano bora ya kibinadamu kutoka kwa bibi Zaharaa (a.s) na kunufaika nayo katika nyanja tofauti za uhai.
  • - Kuingiza elimu ya bibi Zaharaa (a.s) na fikra zake katika maktaba za kimataifa.

Tafiti zitumwe katika anuani ifuatayo: Idara ya shule za dini za wasichana Alkfeel / kituo cha Swaidiqah Twahirah (a.s) / Karbara – mkabala na mtaa wa familia – barabara ya hospitali ya Hussein. Au zitumwe kupitia barua pepe ifuatayo: Fatema14asad@gmail.com

Kwa maelezo zaidi piga namba za simu zifuatazo: (07732840851 / 07602345585).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: