Kutokana na kanuni za ushirikiano: Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Mustanswiriyya wanafanya semina ya kanuni za kuandaa tafiti za kielimu…

Maoni katika picha
Kutokana na kanuni za ushirikiano, Atabatu Atabasiyya tukufu –kupitia maktaba na Daru Makhtutwati ya Atabatu Abbasiyya tukufu- kwa kushirikiana na chuo cha Mustanswiriyya (kitengo cha taaluma na maktaba) wanafanya semina ya kanuni za kuandaa tafiti za kielimu, washiriki wa semina hii ni jopo la watumishi wa vituo na idara za maktaba, kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kufanya utafiti wa kielimu na kuwafanya wawe watalamu zaidi katika uandishi wa tafiti za kielimu.

Semina imeanza Juma Pili (5 Agosti 2018m) katika ukumbi wa Imamu Qassim (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu na itaendelea kwa muda wa siku nne, ipo chini ya usimamizi wa dokta Azhaar Zaidi Jaasim mjumbe wa kamati ya walimu katika kitengo cha taaluma na maktaba kwenye kitivo cha lugha katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya, yatafundishwa mambo muhimu kuhusu namna ya kuandaa utafiti wa kielimu, kuanzia vifaa vya kuchagua, kuchagua anuani, kubaini tatizo na kuangalia namna ya kulitatua, muundo wa utafiti, aina za utafiti kama somo la kwanza, masharti ya ufundi katika kuchagua njia na kuweka vielelezo, pamoja na maswali ya kuuliza katika utafiti wa kielimu, namna ya maswali na malengo yake, vilevile watafundishwa namna ya kutumia teknolojia za kisasa katika maktaba za kawaida na zile za kielektronik, pamoja na mada zingine zitakazo changia kumnufaisha mshiriki na kumfanya apate elimu zaidi.

Dokta Azhaar Zaidi Jaasim ameonyesha furaha yake kutokana na kufanyika kwa semina hii, amesema kua: “Hakika hii sio semina ya kwanza, kuna semina nyingi tumefanya kwa kushirikiana kwa ajili ya kubadilishana uzowefu baina ya kitengo cha taaluma na maktaba katika kitivo cha lugha, kwenye chuo kikuu cha Mustanswiriyya na maktaba, pamoja na Daru Makhtutwati ya Atabatu Abbasiyya tukufu, tumesha soma mada nyingi, katika sekta ya uhakiki, ukarabati, faharasi na zinginezo, hadi kufikia kufanya semina hii ya kuandaa tafiti za kielimu, ni kwa sababu watumishi wa maktaba wamesha piga hatua kubwa katika sekta hii, na wameshiriki katika majadiliano mengi ya kiutafiti, na hili lilikua ni hitaji muhimu baada ya kupiga hatua kubwa katika sekta hiyo, tunatarijia semina hii iwe na matokeo mazuri na iwanufaishe zaidi washiriki”.

Washiriki wa semina wameridhishwa na mada zinazo wasilishwa na zitakazo endelea kuwasilishwa katika semina hii, wakatoa wito wa kufanyika zaidi semina hizi ambazo zinamchango mkubwa katika kuboresha utafiti wa kielimu”.

Kumbuka kua semina hii ni sehemu ya kuendeleza ushirikiano baina ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kitengo cha taaluma cha chuo kikuu cha Mustanswiriyya kwa ajili ya kubadilishana mawazo na uzowefu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: