Likiwa na tafiti bora za aina mbalimbali: Limetoka jarida la saba la (Turathi za Hilla)…

Maoni katika picha
Katika muendelezo wa matoleo yake ya mwanzo likiwa na muonekano mpya, hivi karibuni limetoka toleo la saba la jarida la (Turathi za Hilla) chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ambalo ni jarida linalo andika tafiti za kielimu kuhusu turathi za mji wa Hilla, nalo ni moja ya majarida mengi yanayo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya kielimu na kibinadamu.

Toleo la saba limeandikwa tafiti mbalimbali za aina tofauti kutoka kwa watafiti wa sekula wa vyuo vikuu tofauti, kuna tafiti za kihistoria, kilugha, kifiqhi pamoja na taarifa za uhakiki wa nakala kale za Hilla.

Miongoni mwa tafiti zilizopo katika toleo hili ni:

  • - (Mji wa Hilla katika vitabu vya wasiokua waislamu -Mustashriqina- na safari za wageni) utafiti wa Dokta Zuhair Yusufu Alayuwi.
  • - (Nakala kale za Allaamah Hilliy katika maktaba kuu ya Imamu Alhakiim.. sehemu ya pili) utafiti wa Ustadhi Mhakiki Ahmadi Ali Majidi Alhiliy.
  • - (Mashairi ya Abu Saidi Aljawaani Alhilliy) Utafiti wa Dokta Abbasi Haani Aljaraakh.
  • - (Tafsiri za wanachuoni wa Hilla.. utafiti wa kulinganisha baina ya tafsiri mbili teule, Tafsiri Tibyaani ya Ibun Idrisa Alhilliy, na Muhtari wa Tafsiri Qummiy cha Ibun Ataaiqi) vya watafiti wawili: Dakta Muhammad Abbasi Nu’umaani na mwalimu msaidizi Hussein Nawaar.

Pamoja na tafiti zingine za kielimu, kwa atakaye taka nakala ya toleo hili zinapatikana katika vituo vya mauzo ya moja kwa moja vya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika mkoa wa Karbala karibu na mlango wa Kibla wa malalo matukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: