Hivi punde: Ofisi ya Ayatullahi Sayyid Sistani imetangaza kua kesho Juma Tatu ni siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Dhulhijja…

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa dini mkuu Ayatullahi Mtukufu Sayyid Ali Husseini Sistani imetangaza kua kesho Juma Tatu 13 Agosti 2018m ni siku ya kwanza ya mwezi wa Dhulhijja 1439h.

Mtandao wa Alkafeel umepata taarifa hii kutoka katika ofisi ya Muheshimiwa Sayyid Sistani, taarifa inasema kua ofisi hiyo tukufu imethibitisha kuonekana kwa mwezi mwandamo wa Dhulhijja 1439h.

Kutokana na taarifa hiyo siku ya kwanza ya sikukuu ya Idul-Adhha itakua siku ya Juma Tano 22 Agosti 2018m sawa na 10 Dhulhijja 1439h.

Kwa mnasaba huu, mtandao wa kimataifa Alkafeel unatoa mkono wa pongezi kwa umma wa kiislamu na Maraajii wetu watukufu bila kuwasahau wanachuoni wa kiislamu na raia wa Iraq pamoja na wafuasi wote wa Ahlulbait (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atukubalie ibada zetu na ibada zenu na aineemeshe Iraq na watu wake kwa kuwapa amani na utulivu hakika yeye ni mwingi wa kusikia dua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: