Atabatu Abbasiyya tukufu yafungua milango ya kituo cha Afaaf cha kibiashara kwa wananchi…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu alasiri ya Alkhamisi ya leo (4 Dhulhijja 1439h) sawa na (16 Agosti 2018m) imefungua milango ya kituo cha Afaaf cha kibiashara kwa wananchi.

Kituo hiki ambacho ghorofa la tatu limetengwa maalumu kwa ajili ya wanawake kimejengwa katika kiwanja chenye ukubwa wa (2m2.600), na kina ghorofa tatu, kimegawanywa sehemu mbili: sehemu ya maduka, na sehemu ya maofisi na magodauni, kimefungwa mitandao ya kisasa ya (umeme, viyoyozi, zima moto, kamera, tahadhari, intanet, taa na vinginevyo), halikadhalika kituo hiki kinangazi maalumu za kupandishia mizigo na kupandia watu, pamoja na mambo mengine mengi yamekifanya kitoa hiki kua bora zaidi katika mkoa mtukufu wa Karbala.

Mradi wa kituo cha kibiashara cha Afaaf, kilichopo katika barabara kuu ya kitongoji cha Hussein (a.s) mkabala na eneo la kuogelea katika mtaa wa Hussein Al-Aailiy ni moja ya miradi ya kiuchumi ya Atabatu Abbasiyya tukufu unao toa huduma za kibiashara kwa wakazi wa mkoa wa Karbala na mazuwaru watukufu, huu ni mradi mpya unao toa huduma bora na za uhakika za kibiashara, wanauza bidhaa halisi ambazo sio feki kwa bei nafuu sasa umefungua milango yake kwa wananchi, hili ndio jambo kubwa lililo kusudiwa katika kituo hiki kutoa huduma bora za kibiashara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: