Manufaa ya huduma zake: Kituo cha taaluma Alkafeel chafanya nadwa ya kuitambulisha aprication (app) ya Siraaji na yatoa nakala tano bure kwa uongozi wa malezi wa Karbala…

Maoni katika picha
Baada ya kupatikana mafanikio katika aprication (app) mpya ya (Siraaj) kwenye shule kadhaa ndani ya mkoa mtukufu wa Karbala, ambayo ni aprication ya mawasiliano baina ya viongozi wa shule na wazazi wa wanafunzi inayo saidia kuinua kiwango cha ushirikiano baina yao, kupitia dirisha la mawasiliano ya kimtandao kati ya nyumbani na shuleni, kituo cha taaluma Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimeamua kufanya nadwa maalumu ya kuitambulisha aprication hii, kwa ajili ya kuendelea kunufaika na huduma zake zinazo saidia kuokoa muda wa mwalimu na mzazi katika kufuatilia maendeleo ya mwanafunzi kwa kutumia mtandao ambao ni njia inayo endana na maendeleo ya sasa katika sekta ya mawasiliano, pamoja na kutambulisha teknolojia mpya itakayo nufaisha sekta ya malezi na elimu.

Nadwa hii imefanyika ndani ya ukumbi wa Qassim (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka katika ofisi ya malezi ya mkoa wa Karbala, wakiongozwa na mkuu wa kitengo cha kusimamia vipaji Ustadh Jawadi Nasrullah pamoja na idadi kubwa ya manaibu viongozi wakuu na wakuu wa shule mbalimbali za hapa Karbala, walitowa maelezo ya kina kuhusu aprication hiyo na milango iliyomo, na wakabainisha vipengele muhimu vinavyo rahisisha mawasiliano baina ya shuleni na nyumbani, kwa namna ambayo inaendana na maendeleo ya teknolojia ya sasa.

Nadwa ilikua na usikivu mkubwa na michango ya maoni mbalimbali kutoka kwa wahudhuriaji kuhusu aprication hiyo, pamoja na shuhuda mbalimbali zilizo tolewa na wanufaika wa aprication hiyo.

Mwishoni mwa nadwa, kituo cha taaluma Alkafeel kikatoa zawadi ya nakala tano za aprication kwa uongozi mkuu wa malezi wa mkoa mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: