Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa mkakati wa kuimarisha usalama na kuboresha huduma, kwa ajili ya kuwapokea mazuwaru wa siku ya Arafa na usiku wa Idil Adh-ha pamoja na mchana wake, vitengo vya ulinzi na usalama pamoja na vitengo vya kutoa huduma vimefanya vikao mara kadhaa kwa ajili ya kuandaa mkakati huo, na hatua za kwanza za utekelezaji zimeanza leo siku ya Juma Tatu na utekelezaji utaendelea hadi siku ya mwisho ya sikukuu, tunawahakikishia usalama wa hali ya juu na upatikanaji wa huduma bora.
Mkakati huu ni sehemu ya kuendeleza mafanikio yaliyo wahi kupatikana katika matukio ya nyuma, katika matukio hayo kila kitu kilifanyika vizuri, vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu huchukua kila zuri lililo fanyika katika matukio ya nyuma na kuendelea kunufaika nalo, viongozi wa vitengo wamejadiliana mazuri yaliyo fanyika katika matukio ya nyuma, kisha kila kitengo kimewasilisha mkakati wake kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kujadiliwa na kamati za usalama na utumishi, lengo kubwa ni kutoa huduma bora kwa mazuwaru na kuandaa mazingira yatakayo wawezesha kufanya ziara kwa urahisi, vitengo vyote vimejipanga imara kwa ajili ya kuhakikisha vinatoa huduma bora inayo endana na idadi ya mazuwaru watukufu katuka usiku huo mtakatifu.
Kumbuka kua miongoni mwa ziara zinazo fanyika katika Ataba za Karbala na kuhudhuriwa na mamilioni ya watu ni ziara ya siku ya Arafa na Idil Adh-ha, waumini humiminika kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara maalumu ya siku ya Arafa na Usiku wa Idi pamoja na mchana wake.