Kwa picha: Maelfu ya watu waswali Idil Adh-ha tukufu katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Baada ya kuchomoza Alfajiri ya mwezi kumi Dhulhijja (1439h), maelfu ya watu wametekeleza swala ya Idil Adh-ha katika uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), chini ya mazingira bora ya kiroho na mapenzi makubwa ya Mwenyezi Mungu na Mtume pamoja na Ahlulbait (a.s), baada ya halaiki iliyo kuja kutoka ndani na mje ya Iraq kukamilisha ibada maalumu za Arafa wamehitimisha kwa swala tukufu ya Idi.

Uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umeshuhudia zaidi ya swala moja ya Idi, kutokana na wingi wa watu walio kuja kuswali swala hiyo, hali ilikua hivyohivyo katika haram ya bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s) katika utekelezaji wa swala ya Idi.

Fahamu kua swala ziliswaliwa ndani ya uwanja wa haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), na katika uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu ulio kuwa na watu wengi zaidi na kuongozwa na Mheshimiwa Shekh Habibu Alkaadhimiy.

Waumini wamejikurubisha kwa Mwenyezi Mungu na kumuomba auneemeshe umma wa kiislamu na ulimwengu kwa ujumla kwa kuupa amani na usalama, na aijaalie Iraq ipate amani na utulivu, na aferishe njama za makafiri na maadui wa Iraq, awadhalilishe na kuvunja umoja wao, azinyanyue bendera za wapiganaji wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, awarehemu mashahidi wa Iraq na awaponye haraka majeruhi.

Kumbuka kua Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimefanya kila ziwezalo katika kuwapokea mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa siku kadhaa, na kuwapa huduma bora, vyombo vya ulinzi na usalama na vituo vya afya vya Karbala waliimarisha huduma zao kwa ajili ya kudhibiti usalama na uboreshaji wa huduma kwa mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: