Katika nchi (110): Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu imehudhuria katika kongamano kubwa la kimataifa kuhusu maktaba na taaluma…

Maoni katika picha
Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika kongamano la kimataifa la themanini na nne kuhusu maktaba na taaluma, linalo ratibiwa na umoja wa jumuiya na taasisi za maktaba (Ifla) katika mji mkuu wa Malezia, chini ya kauli mbiu isemayo: (Kubadilisha mwenendo wa maktaba ni njia ya kubadilisha jamii), linalo angalia athari za makataba katika kubadilisha jamii na umma, ambalo zimeshiriki zaidi ya nchi (110) na kuhudhuriwa na watu zaidi ya (3500).

Ushiriki wa maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu ni wa mara ya kwanza katika kongamano hili, ushiriki huu ni fursa ya kuonyesha maendeleo yake katika sekta ya maktaba na namna inavyo endana na kanuni za kielimu katika sekta hiyo, kwa msingi kuo ilikubali kushiriki ili ionyesho maendeleo yake na iangalie namna maktaba zingine za kimataifa zinavyo fanya, sambamba na kuonesha picha kua Iraq ni nchi ya kielimu pamoja na changamoto inazo pitia.

Pamoja na kuhudhuria katika kongamano hili na kuangalia uzowefu wa wengine katika sekta hii, imeteuliwa kua miongoni mwa wazungumzaji (64) wanao wakilisha nchi (32), na wamechaguliwa kuongea mada isemayo: (Nafasi ya maktaba za Iraq baada ya Daesh) hii ni nafasi muhimu sana kwa maktaba za Iraq.

Kumbuka kua kongamono hili (Ifla) linamada nyingi, na linahudhuriwa na wasomi wengi walio bobea katika mambo ya maktaba kutoka kila sehemu ya dunia na hufanywa kila mwaka, huratibiwa na taasisi za maktaba na taaluma wanachama wa (Ifla), pamoja na jumuiya ya maktaba za Malezia, na hufadhiliwa na wizara ya utalii na utamaduni ya Malezia pamoja na maktaba za malezia, ushiriki wa maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho na kongamano hili ni wa mara ya kwanza kwa taasisi za Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: