Mbele ya malalo yake takatifu, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanahuisha utiifu wao kwa baba yake Kiongozi wa Waumini (a.s) katika Idi Ghadiir…

Maoni katika picha
Katika eneo ambalo ni kilele cha utukufu na uaminifu haram ya mtoto wa aliye tangazwa katika eneo la Ghadiir Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwa ni sehemu ya kuonyesha furaha yao kutokana na tukio hili la sikukuu kubwa na tukio muhimu kwa waislamu, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wamehuisha utiifu wao kwa Wasii wa Mtume Mtukufu (s.a.w.w).

Ni kawaida ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kila siku ya Juma Nne na Alkhamisi kufanya ibada maalumu na kuonyesha utiifu kwa Maimamu, lakini kuna siku zina matukio maalumu ikiwemo siku ya sikukuu kubwa ya Mwenyezi Mungu ambayo imesadifu leo (18 Dhulhijja 1439h), baada ya kumaliza ibada ya ziara wakiwa wamesimama kwa mistari mbele ya kaburi lake takatifu huku wamebeba mauwa, kama ishara ya kuonyesha furaha yao, na wakiimba kaswida za utiifu zilizo jaa maneno yanayo onyesha utukufu wa tukio hili, pamoja na kutoa pongezi kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na kumbukumbu hii tukufu.

Katika furaha hii na kutoa salamu kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kuhuisha utiifu wao kwa baba yake (a.s), kundi kubwa la mazuwaru watukufu wameshiriki pamoja nao.

Kumbuka kua sikukuu ya Idi Ghadiir ni sikukuu kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu nayo ndiyo sikukuu kubwa zaidi kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), hakuna Mtume yeyote ispokua alisherehekea siku hii na aliiheshimu, siku hii mbinguni inaitwa (siku ya ahadi iliyo ahidiwa) na hapa duniani inaitwa (siku ya ahadi iliyo tekelezwa na kundi lililo shuhudiwa).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: