Rais wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu: Kuna njia mbili, Njia sahihi inayo mjenga mwanadamu, na njia isiyo sahihi inayo mbomoa mwanadamu huku akifikiri kua anajijenga yatupasa kuchagua kwa makini…

Maoni katika picha
Katika hatua ya pili ya (PDC): Kwenye hafla ya kuhitimisha ratiba ya mafunzo ya kujenga uwezo yaliyo andaliwa na jumuiya ya Skaut ya Alkafeel ambayo iko chini ya idara ya watoto na makuzi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, iliyo andaliwa kwa viwango vya Skaut vya (Ashbaal, Alkashaafah na Aljawaal) kwa vijana wenye umri wa miaka tisa hadi kumi na nane, kulikua na ujumbe kutoka katika kitengo cha habari na utamaduni ulio wasilishwa na rais wa kitengo hicho Sayyid Liith Mussawi, alianza kwa kutoa pongezi za Idi Ghadiir, kisha akasema kua: “Nawapongeza kwa kuhitimu hatua hii ya kujenga uwezo iliyo andaliwa na ndugu zetu wa idara ya watoto na makuzi, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu ajalie mafunzo haya yawe na faida kwa watoto wetu walio shiriki katika program hii”.

Akaongeza kua: “Napenda nibainishe lengo la kujenga uwezo, tunakusudia nini tunaposema kujenga uwezo? Bila shaka tunakusudia kujenga uwezo wa mtu, hakuna asiyejua kuwa uwezo wa mtu ni maumbile ambayo Mwenyezi Mungu amempa kila mwanadamu, kila mtu anatakiwa aendeleze uwezo wake, tatizo ambalo linawapata watu wengi hukosea njia ya kuendeleza uwezo wao, kuna njia mbili, njia sahihi inayo muwezesha mwanadamu kujenga uwezo wake, na njia isiyo sahihi ambayo mwanadamu anaweza kudhani anajenga uwezo kumbe anajiangamiza, kwa hiyo tatizo kubwa lipo katika kuchagua njia sahihi itakayo mpa mafanikio mwanadamu, kuna hatua za kufuata hadi mwanadamu afike katika mafanikio”.

Akabainisha kua: “Hakika ndugu zetu wa idara ya watoto na makuzi kupitia ofisi ya hema za Skaut, wametoa mafunzo mbalimbali kwa vijana wakiume na wakike yatakayo wasaidia katika maisha yao, na kuwawezesha kuendeleza uwezo wao, katika nyanja tofauti, katika swala la kujitambua na kuweza kupangilia mambo mazuri kwa mustakbali wao, kuna masomo mengi ambayo yanaweza kumsaidia kijana akaweza kuendeleza uwezo wake, kwa bahati mbaya, upande mwingine tunaona kuna kijana anayetaka kuendeleza uwezo wake lakini kakosea njia, kwa sababu anaamini kuna vitu akivipata ataendelea, na ukweli vitu hivyo vinamuweka mahala pabaya na kupunguza uwezo wake, na haangalii mambo yanayo weza kumpa nguvu”.

Akaendelea kusema kua: “Watu wengi hutamani vitu vya thamani katika maisha yao, vitu vya thamani ni msingi wa kufeli, muonekano na kujionyesha husababisha utu apite njia mbaya, na baada ya muda mtu huyo hujikuta kawa duni katika jamii, yawezekana kwa ajili hii ndio tunaona baadhi ya mambo yasiyo faa katika jamii yetu, ndio maana jumuiya ya Skaut wameweka ratiba ya kimalezi ambayo inawaelekeza vijana wetu na mabinti zetu namna ya kuendeleza uwezo wao, mipango yote pamoja na ratiba viko chini ya bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ukizingatia kua jumuiya hii ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, juhudi kubwa zinafanyika kuhakikisha vijana na mabinti zetu wanakua watu bora katika jamii kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Wazazi wa vijana walioshiriki katika Skaut akawaambia kua: “Naziomba familia zetu tukufu ziongeze juhudi ya kuwahimiza watoto wao kushiriki katika hema hizi, masomo haya na hema hizi sio kwamba hupatikana wakati walikizo za kiangazi peke yake, zipo hema ambazo huandaliwa katika vipindi vingine na katika matukio ya Ahlulbait (a.s), wasimamizi wa masomo haya wameweka ratiba mbalimbali ambazo wazazi mnatakiwa kuwaleta watoto wenu, sio mkae mnasubiri likizo za kiangazi peke yake, waleteni pia katika matukio mengine. Tunamuomba Mwenyezi Mungu akilinde kizazi chetu, watoto wetu na familia zetu, na awape nguvu wasimamizi wa ratiba hii, na amlinde kila aliye changia katika ratiba hii, bila kuwasahau ndugu zetu wa Mujamma’a Sheikh Kuleini (r.a), walikua msaada mkubwa katika kipindi chote cha mafunzo haya na bado wanaendelea kusaidia hadi mwisho wa ratiba”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: