Kukamilika jengo jipya la Maahadi ya Qur’an tawi la wanawake katika mji wa Najafu Ashrafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu wamemaliza ujenzi wa jengo jipya la Maahadi ya Qur’an tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, likiwa na ubora unao endana na kazi tukufu ya Maahadi, miongoni mwa harakati za Qur’an.

Ujenzi wa jengo hili umetokana na upanuzi wa Maahadi ya Qur’an tawi la wanawake, jengo la zamani lilikua halimudu harakati za Qur’an zinazo tolewa, hivyo uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya ukaamua kujenga jengo lingine katika sehemu inayo faa, ndipo kitengo cha usimamizi wa kihandisi kikapawa jukumu la kubuni na kujenga bila kutegemea nguvu za nje.

Tumeongea na rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi Muhandisi Abbasi Mussa kuhusu mradi huu, ambaye amesema kua: “Baada ya kupewa jukumu na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu la kujenga, tulianza kuandaa mchoro wa ramani ya jengo, na baada ya kupasishwa mchoro huo tukaanza ujenzi moja kwa moja kwa kufuata mchoro huo ambao unaendana moja kwa moja na mahitaji ya Maahadi tawi la wanawake, tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumekamilisha ujenzi ndani ya muda ulio pangwa na bila kuomba msaada kutoka sehemu yeyote ya nje, kazi zote zimefanywa na wataalamu wetu, idara ya ujenzi, idara ya miradi ya nje, idara ya umeme na idara ya viyoyozi”.

Mhandisi msimamiaji wa mradi bwana Hassanaini Alaa Aali-Shabbir akaongeza kusema kua: “Ujenzi umefanyika katika eneo la (mtaa wa Karaama) ndani ya mkoa wa Najafu Ashrafu kwenye kiwanja chenye mita za mraba (300) likiwa na ghorofa tatu, ghorofa la kwanza lina sehemu za mapokezi na ofisi tofauti pamoja na chumba cha mitambo ya spika, na vyumba vitano vya madarasa, ghorofa la pili lina chumba cha kupumzika na chumba cha kulelea watoto pamoja na vyumba saba vya madarasa, na ghorofa la tatu lina ukumbi wa mikutamo”.

Akaongeza kua: “Jengo hili lina ngazi ya lifti pamoja na ngazi za kawaida, vile vile lina maji, umeme, sehemu ya vyoo, viyoyozi, vifaa vya zima moto, vifaa vya mawasiliano, spika na kamera, wakati wa kumalizia mradi huu tumeweka mapambo mazuri yanayo endana na maendeleo ya kisasa”.

Tunapenda kusema kua, kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitengo muhimu, kina idara nyingi na mafundi pamoja na wahandisi wanao fanya kazi usiku na mchana katika sekta zote za ndani na nje ya Ataba tukufu kwa ajili ya kuhakikisha inatoa huduma bora kwa mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: