Muhimu.. Kwa agizo rasmi la Marjaa Dini mkuu: Mheshimiwa Sayyid Swafi awasili Basra na ujumbe wa wataalamu kwa ajili ya kuchunguza tatizo na kutafuta ufumbuzi haraka wa muda mfupi na muda mrefu…

Maoni katika picha
Kutokana na agizo la Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu Ashrafu, wakili wake ambaye ni kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na ujumbe wa wataalamu wamefanya ziara katika mkoa wa Basra, kwa ajili ya kuwasaidia watu wa mkoa huo na kubaini tatizo pamoja na kutafuta ufumbuzi haraka wa muda mfupi na muda mrefu hususan tatizo la maji chumvi na ukosefu wa maji safi, ugeni huo umebainisha kua hauta ondoka hadi wajue kiini cha tatizo na namna ya kulitatua.

Marjaa Dini mkuu kupitia khutuba za Ijumaa alikua amesha zungumzia umuhimu wa kutatua tatizo la ukosefu wa maji safi katika mji wa Basra, na akasisitiza kua vyombo vinavyo husika hawafanyi juhudi yeyote ya kutatua tatizo zaidi ya kutupiana lawama, habari kutoka katika mji wa Basra zinasema kua maji machafu yanayo tumiwa na watu wa Basra yamesha dhuru mamia ya wakazi walio ripotiwa na hospitali ya mkoa katika siku za nyuma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: