Mwakilishi wake akiongeo kutoka Basra: Marjaa Dini mkuu ametuagiza kuja Basra kusaidia utatuzi wa tatizo la maji hakuta ukweli wa habari zinazo sambazwa tofauti na hii…

Maoni katika picha
Mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi leo ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua, hajazungumza kitu chochote rasmi tangu alipo wasili pamoja na jopo la wataalamu katika mji huo kwa ajili ya kuangalia utatuzi wa tatizo la maji katika mkoa wa Basra.

Akabainisha kua: “Tumeagizwa na Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Sistani kwa jukumu maalumu, ambalo ni kuwasaidia ndugu zetu wakazi wa Basra kumaliza tatizo kubwa walilo nalo la ukosefu wa maji, tunafanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya kutatua tatizo hilo kwa muda mfupi, wakati na mrefu, tumeanza kufanya kazi kwa vitendo kwa kadri ya uwezo wetu”

Akaongeza kua: “Katika jambo hili tunamwakilisha yeye na sio Atabatu Abbasiyya tukufu”. Akafafanua kua: “Hakuna ukweli wa yale yanayo sambazwa na mitandao ya kijamii kuhusu maeneo au matamko au madai mengine, fahamuni kua sisi hatuna ukurasa au luninga katika toghuti yeyote miongoni mwa mitandao ya kijamii”.

Muheshimiwa (Sayyid Ahmadi Swafi) aliondoka Najafu tangu (02/09/2018) akiwa na jopo la watalamu kwa amri ya Marjaa Dini mkuu kwenda kusaidia utatuzi wa tatizo la maji linalo wasumbuwa wakazi wa mji wa Basra.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: