Mtandao wa kimataifa Alkafeel waelezea juhudi zinazofanywa na jopo la wataalamu walio kwenda kusaidia kuondoa tatizo la maji katika mji wa Basra kutokana na agizo la Marjaa Dini mkuu…

Maoni katika picha
Muhandisi Dhiyau Majidi ambaye ni mmoja wa wataalamu walio fuatana na mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi kutafuta ufumbuzi wa tatizo la maji katika mji wa Basra, amesema kua: “Hakika kwa baraka za Mwenyezi Mungu mtukufu, tumeanza hatua za kwanza za kurejesha maji katika mji wa Basra, tumefanya makubaliano na shirika moja kwa ajili ya kufunga mashine za kusukuma maji katika kituo cha maji cha Albid’ah ambacho husambaza maji katika vituo vingine (RO) kina maji asilia na mazuri”.

Akaongeza kua: “Tulipo fika katika mkoa huu tulifanya vikao vingi na wahusika mbalimbali, kisha tukaelekea katika kituo cha maji kwa ajili ya kuweka mikakati ya kuondoa tatizo, baada ya kufanya upembuzi yakinifu katika kituo hicho na kukagua mashine za kusukuma maji zilizopo, chini ya usimamizi wa mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, tukagundua tatizo kubwa ni kutelekezwa na kinafanya kazi kwa kiwango kidogo sana tofauti na kilivyo pangiwa, baadhi ya vituo vilikua havifanyi kazi kwa sababu ndogo sana, kwa mfano kukosekana mtu wa kubadilisha kifaa tu”.

Akafafanua kua: “Utatuzi upo wa aina mbili, kwanza: Kuongeza ukubwa wa hodhi la maji kutoka sehemu yanapo chukuliwa, kutoka mita (7) urefu wa kwenda juu hadi mita (9), na siku za mbele zitakua mita (10).

Pili: Kufanya makubaliano na moja ya mashirika ya Iraq kwa ajili ya kufunga mashine za kusukuma maji zipatazo (18), tayazi sehemu ya mashine hizo zimesha letwa na zingine zinaendelea kuletwa, ndani ya muda mfupi kituo hiki kitaanza kufanya kazi kwa uwezo wake wote, pia tumetengeneza mashine zilizo kuwepo, tumezisafisha na kubadilisha vifaa vilivyo haribika”.

Akabainisha kua: “Kituo mwenza kinacho peleka maji katika kituo cha Albid’ah, kimefanyiwa matengenezo pia, kimesafishwa na kubadilishwa mashine za kusukuma maji pamoja na kufungwa vifaa vingine vilivyo hitajika ili kukiwezesha kufanya kazi, na tumetengeneza sehemu zote zenye vituo vinavyo tumika kusambaza maji kwa wakazi wa eneo la karibu na kituo hiki”.

Tunapenda kukumbusha kua, baada ya tatizo la ukosefu wa maji safi katika mji wa Basra, Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu Ashrafu ametuma ujumbe ukiongozwa na mwakilishi wake Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi pamoja na jopo la wataalamu kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa haraka (wa sasa), wa muda wakati na muda mrefu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: