Kwa picha: Mawaakibu za kuomboleza zimeanza kuwasiri asubuhi ya siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam 1440h…

Maoni katika picha
Baada ya kuchomoza asubuhi ya siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Muharam katika mazingira ya huzini, Mawaakibu za kuomboleza zimeanza matembezi ya Ashura wakitoa pole na taazia kwa Imamu wa Zama (a.f) kwa kifo cha bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), Mawaakibu zimemiminika katika malalo mawili matukufu zikiwa zimejaa huzuni.

Uingiaji wa Mawaakibu katika Ataba mbili tukufu ulifuata ratiba iliyo andaliwa na kitengo cha maadhimisho na Mawaakibu pamoja na vikundi vya Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu kilicho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, zinaingia katika kaburi tukufu la Abulfadhil Abbasi (a.s) kupitia mlango wa Kibla kisha wanafanya maombolezo na kujipiga vifua huku wanalia kudumisha msiba wa milele, kisha wanatokea mlango wa Imamu Hussein (a.s) na kuelekea katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu halafu wanakwenda katika malalo ya bwana wa mashahidi Abul Ahraar (a.s), huku wakiimba kaswida za kuomboleza na kupiga vifua njia yote hadi wanaingia katika uwanja wa haram ya Imamu Hussein (a.s), huku nyoyo zao zikiwa zimejaa mapenzi ya Hussein, akili zao zimemuelekea Hussein, ndimi zao zinatamka Hussein, Hussein, na kuhuisha utiifu wao kwa mjukuu wa Mtume na kipenzi chake na bwana wa vijana wa Peponi (a.s).

Tunapenda kufahamisha kua, kutokana na wingi wa Mawaakibu zilizo omba kushiriki katika maombolezo ya siku kumi za mwanzo wa Muharam, imelazimika kuwa na mimbari nyingi katika uwanja wa haram tukufu ya Abbasi, ili kila Maukibu ipate nafasi ya kutafuta ujira na thawabu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: