Miongoni mwa Maswahaba wa Mtume walio uwawa mbele ya Imamu Hussein (a.s) ni Anasi bun Kaahil Asadiy…

Kaburi la Shahidi
Neno “Swahaba” hutumika kwa wale walio kutana na Mtume (s.a.w.w) au walio pokea hadithi kutoka kwake, au walio ishi naye kwa kipindi fulani, na linapo tumika kwa Imamu miongoni mwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) husemwa: Miongoni mwa Maswahaba wa Amirul Mu-uminina (a.s), au Maswahaba wa Hassan (a.s) au Maswahaba wa Hussein (a.s), katika Maswahaba wa Imamu Hussein (a.s) kulikua na baadhi ya Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w) miongoni mwao ni Anasi bun Kaahil Asadiy, ambaye ni Swahaba mtukufu aliye shuhudia vita ya Badri na Hunain pamoja na vita ya Karbala.

Jina lake kamili ni; Anasi bun Haarith bun Kaahil bun Amru bun Swa’abu bun Asadi bun Khuzaimata Al-Asadiy Al-Kaahiliy, alikua miongoni mwa viongozi wa Kufa na miongoni mwa wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s), alikua mzee sana na Swahaba mtukufu wa Mtume (s.a.w.w), alisikia hadithi kutoka kwa Mtume na alishuhudia vita ya Badri na Hunain.

Alionyesha mapenzi yake kwa watu wa nyumba ya Mtume kwa kujitolea nafsi yake kwa ajili ya kumnusuru Hussein (a.s), Bukhali anasema: miongoni mwa hadithi alizo pokea kutoka kwa Mtume anasema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) anasema na Hussein (a.s) akiwa miguuni kwake: (Hakika mtoto wangu huyu atauwawa katika ardhi ya Karbala huko Iraq atakaye shuhudia aende akamnusuru).

Alikutana na Imamu Hussein usiku wakati akija Karbala, ametajwa na Shekh Muhammad Mahdi Shamsu Dini. Na ametajwa na Sayyid Khui (r.a): wakampasisha kua ni (Anasi bun Kaahil Asadiy) aliye tajwa katika ziara ya Rajabiyya (mwezi wa Rajabu), Sayyid Khui akapasisha kua utambulisho wake kamili ni Alkaahiliy Asadiy, jina la ibun Kaahili linatokana na ukoo, ametajwa pia na ibun Shahru Aashubu na Khawarzamiy kwa jina la (Maaliki bun Anasi Alkaahiliy), na ametanjwa na Shekh Majlisi katika kitabu cha Bihaari kwa jina hilo hilo la (Maaliki bun Anasi Alkaahiliy) kisha likasahihishwa na ibun Namaa Alhilliy.

Banu Kaahil wanatokana na bani Asadi bun Khuzaimata bun Adnani (Waarabu wa kaskazini). Alikua na umri mkubwa sana na miongoni mwa Maswahaba wenye heshima kubwa katika mji wa Kufa, Ibun Saadi ametaja kuwa katika mji wa Kufa kulikua na nyumba za bani Kaahil.

Mchango wake katika vita ya Twafu: Swahaba huyu mtukufu Anasi bun Haarith (r.a) alimuomba ruhusa Imamu Hussein (a.s) ya kwenda kupigana na maadui, Imamu akamruhusu. Alipigana hadi akauwawa katikati ya maadui, Imamu Hussein (a.s) alipo muangalia alitokwa na machozi na akasema: Mwenyezi Mungu anakushukuru ewe mzee, aliingia katikati ya uwanja wa vita akiwa anachechemea:

Alitambua Kaahilu kisha Dudaani…. Na Khandafiyyuuna na Qaisu Ilaani.

Ya kwamba umma wangu umesha kufa…… Na mimi ni bwana wa majemedari.

Alipigana vita ya kishujaa, aliuwa maadui kumi na nane pamoja na uzee wake, kisha ndio akazidiwa na roho yake ikatoka na kwenda kwa Mola wake Peponi pamoja na Mitume na wasadikishao na mashahidi watukufu, hakika hao ndio marafiki wema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: