Inatokea hivi sasa Karbala…

Maoni katika picha
Sehemu: Karbala tukufu mji wa mashahidi na kujitola.

Siku: Alkhamisi mwezi tatu Muharam 1440h.

Tukio: Ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kuhuisha maombolezo ya Ashura.

Mtu anaye kuja katika mji wa Karbala ndani ya siku hizi atakutana na huzuni na maombolezo, pindi tu miguu yake itakapo kanyaga eneo hili tukufu moyo wake utaingia majonzi na atashuhudia matukio mbalimbali ya kuomboleza tukio la Ashura, eneo hili limekua ni kielelezo cha huzuni za kudumu kwa wageni wa Mwenyezi Mungu mtukufu kutokana na yaliyo wapata watu wa nyumba ya Mtume (a.s), na kitaendelea kua kituo cha majonzi katika nyoyo safi hadi siku ya kiyama, tunaweza kueleza kwa ufupi katika nukta zifuatazo hasa maeneo yanayo zunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ambayo ni kilele cha machungu ya maombolezo ya Ashura.

  • - Usiku wa Ijumaa katika kila wiki hushuhudia idadi kubwa ya mazuwaru, lakini baadhi ya siku idadi huwa kubwa zaidi kutokana na matukio (minasaba) maalumu, zikiwemo siku kumi za kwanza katika mwezi wa Muharam, kwa ajili ya kutafuta utukufu wa siku hizo kwa kuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuonyesha unyenyekevu wao kwa Ahlulbait (a.s).
  • - Mawaakibu za kuomboleza zimeendelea kumiminika katika malalo ya Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) zikija kuhuisha utiifu na kudumisha mwenendo wa Imamu Hussein pamoja na kushikamana na malengo ya harakati yake tukufu huku wakiimba mimbo ya kuomboleza tukio la Ashura, na mazingira yakijieleza wazi kua: (Katu yaa Zaharaa hatutamsahau Hussein).
  • - Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na watumishi wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu wanafanya kila wawezalo kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma bora zinazo endana na wingi wa mazuwaru, na kuwafanya watekeleze ibada zao kwa amani na utulivu ikiwemo kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • - Watumishi wa kitengo cha Mawaakibu na maadhimisho ya Husseiniyya wamebeba jukumu la kuratibu matembezi ya mawaakibu Husseiniyya ili wasisababishe usumbufu kwa mazuwaru au baina yao, wanatembea kwa mpangilio mzuri kwa kufuata ratiba maalumu.
  • - Eneo la jirani na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) limejaa Mawaakibu zinazo toa kuhuma kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: