Miongoni mwa maswahaba walio uwawa pamoja na Imamu Hussein (a.s) ni swahaba mtukufu Kinana bun Atiiq Ataghlabiy…

Maoni katika picha
Neno “Swahaba” hutumika kwa wale walio kutana na Mtume (s.a.w.w) au walio pokea hadithi kutoka kwake, au walio ishi naye kwa kipindi fulani, na linapo tumika kwa Imamu miongoni mwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) husemwa: Miongoni mwa Maswahaba wa Amirul Mu-uminina (a.s), au Maswahaba wa Hassan (a.s) au Maswahaba wa Hussein (a.s), katika Msafara wa Imamu Hussein (a.s) kulikua na baadhi ya Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w) miongoni mwao ni Kinana bun Atiiq Ataghlabiy.

Abu Ali anasema: Kinana bun Atiiq Ataghlabiy alikua miongoni mwa wafuasi wa Imamu Hussein (a.s) na aliuwawa pamoja naye Karbala. Asqalaani anasema katika kitabu chake cha Al-Iswaaba: jina lake ni Kinana bun Atiiq bun Muawiyya bun Swaamit bun Qais Ataghlabiy Alkuufiy, alishuhudia vita ya Badri yeye pamoja na baba yake Atiiq mpiganaji wa Mtume (s.a.w.w).

Ibun Uqda amemtaja katika historia yake, na Almmah amesema katika khulaswah: Kinana bun Atiiq bun Muawiyya bun Swaamit, mpiganaji wa Mtume (a.s.w.w), wanachuoni wa historia wanasema: Kinana bun Atiiq alikua miongoni mwa makomando wa mji wa Kufa, alikua mcha Mungu, msomaji wa Qur’an, alikuja kumnusuru Imamu Hussein (a.s) katika siku za mitihani, akapigana hadi akauwawa, muandishi wa kitabu cha Hadaaiq amepokea kutoka kwa Ahmadi bun Muhammad Sarawiyyu kua amesema: Kinana bun Atiiq alikua katika kundi la watu wa kwanza kuuwawa. Na wengine wanasema: Aliuwawa katika mapigano ya kwanza yaliyo fanyika kabla ya swala ya Adhuhuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: