Wajukuu wa Imamu Hussein (a.s) miongoni mwa watumishi masayyid wanahuisha usiku wa kumi wa Muharam…

Maoni katika picha
Usiku wa mwezi kumu Muharam ni tofauti na siku zingine za Ashura, kuna mawaakibu nyingi ambazo huomboleza katika usiku huu, miongoni mwa mawakibu hizo, ni maukibu ya watumishi masayyid ambao ni wajukuu wa Imamu Hussein (a.s) wanao fanaya kazi katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na wasio fanya kazi katika Ataba hizo.

Imekua desturi na mazowea waliyo rithi kizazi baada ya kizazi, kufanya matembezi wakiwa wamevaa vilemba vya kijani, vilivyo zungushwa katika kofia nyekundu, wakitanguliwa na bango huku wakiimba kaswida na mashairi ya huzuni na kuomboleza msiba wa babu yao Imamu Hussein (a.s), hukusanyika sehemu maalumu na hutanguliwa na wazee pamoja na viongozi wao wa kifamilia miongoni mwa familia za Karbala, hushirikiana na watoto wao pamoja na kundi la mazuwaru.

Kumbuka kua maukibu ya Masayyid ambao ni watumishi wa Ataba mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) ni miongoni mwa maukibu kongwe hapa Karbala, iliundwa baada ya uhuru wa taifa la Iraq mwaka wa (1921m), iliendelea kuimarika mwaka baada ya mwaka kutokana na mazingira yaliyo kuwepo, maombolezo haya pamoja na baadhi ya maadhimisho mengine yalipigwa marufuku na utawala uliopita (utawala wa Sadam), marufuku hiyo iliendelea hadi ulipo anguka utawala huo mwaka wa (2003m), ndipo maombolezo haya yakarudi tena kama yalivyo kuwa mwanzo, na hufanyika usiku wa mwezi kumi Muharam kila mwaka, yanahusisha familia za Masayyid walio fanya kazi katika Ataba mbili tukufu pamoja na wajukuu zao wanao fanya kazi hivi sasa katika Atabatu Husseiniyya na Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: