Mwaka wa pili wa kuigiza: kamati ya Zaharaa (a.s) waigiza yaliyo jiri mwezi kumi Muharam…

Maoni katika picha
Mwaka wa pili mfululizo na kwa kuwasiliana na kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya cha Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kamati ya Zaharaa (a.s) katika mkoa wa Diwaniyya asubuhi ya leo (12 Muharam 1440h) wamefanya maigizo ya kuonyesha yaliyo jiri Karbala mwezi kumi Muharam kwa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) pamoja na maswahaba wake, igizo hilo limefanyikia katika kiwanja kilichopo katika barabara ya (Najafu – Karbala).

Bwana Haadi Atwishaan Shamraan ambaye ni kiongozi wa kamati ya Zaharaa (a.s) ya kutoa huduma, ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kwa mwaka wa pili kamati ya Zaharaa (a.s) inafanya igizo la tukio la Twafu katika ardhi ya Karbala tukufu, tukio linalo onyesha kudhulumiwa kwa Imamu Hussein (a.s) na maswahaba wake na yaliyo jiri mwezi kumi Muharam mwaka (61h), maandalizi ya igizo hili yalianza tangu miezi sita iliyo pita, baada ya kupata kibali kutoka katika uongozi wa mkoa wa Karbala pamoja na kitendo cha mawakibu Husseiniyya cha Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, tulianza kuandaa mahema na kufanya mazowezi ya uigizaji, kazi hii ilianzia katika mji wa Ghammaas, na mwaka huu tukapanga igizo hili tulifanyie katika ardhi tukufu ya Karbala, ardhi ya shahada na utukufu”.

Akaongeza kua: “Idadi ya watu wanao igiza upande wa jeshi la Umawiyya wanafika (1200), na watu wanao igiza upande wa Imamu Hussein ni (72), pamoja na kundi la wanawake na watoto, na maneno wanayo ongea tumeyahakiki kupitia wanachuoni na watafiti wa mji wa Najafu Ashrafu”.

Kumbuka kua maonyesho ya igizo hili yamehudhuriwa na watu wengi na kufuatiliwa kwa karibu na watu walio kuja kutoka ndani na nje ya mkoa mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: