Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wamalizia kusafisha haram na uwanja wake mtukufu…

Maoni katika picha
Baada ya makundi ya mazuwaru kumaliza rasmi ziara ya Ashura katika siku ya kumi Muharam, na maombolezo maalumu yaliyo fanyika ya kumbukumbu ya Ashura yaliyo dumu kwa zaidi ya siku kumi, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu na idara ya watumishi ambao ni Masayyid pamoja na walio saidia kutoka katika vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya usafi katika haram na uwanja wake mtukufu.

Wametumia wakati wa usiku mkubwa kufanya kazi hii kutokana na uchache wa mazuwaru katika mida hiyo, kazi hiyo imejumuisha kutandua kapeti lililotandikwa siku chache kabla ya ziara, pamoja na kuondoa michanga na vumbi kisha kazi ya usafi ilianzia ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi katika uwanja wake na milangoni, baada ya hapo yakatandikwa mazuria yaliyo kuwepo mara ya kwanza na hali imerudi kama ilivyo kua kabla ya siku za ziara.

Kumbuka kua vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya kumaliza ziara ya mwezi kumi Muharam na baada ya kutangaza mafanikio ya mkakati zake za ulinzi na utowaji wa huduma, walianza hatua ya pili ya utendaji wao, iliyo husisha kufanya usafi katika maeneo ya ndani na nje ya Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: