Yanajiri hivi sasa: Makabila na koo za wairaq zikitanguliwa na kabila la bani Asadi wanahuisha kumbukumbu ya kuzikwa miili mitakatifu ya mashahidi wa Twafu…

Maoni katika picha
Mji mtukufu wa Karbala leo (13 Muharam 1440h) sawa na (23 Septemba 2018m) umeshuhudia mawakibu za makabila ya Iraq zikitanguliwa na kabila la bini Asadi wakihuisha kumbukumbu ya kuzikwa mwili mtakatifu wa bwana wa mashahidi na watu wa nyumbani kwake (a.s) pamoja na maswahaba wake wema walio uwawa katika vita ya Twafu mwaka wa 61h.

Mawakibu hizi zilianzia matembezi yao karibu na malalo ya bwana wa uzuri (Sayyid Juudah) mashariki ya mji wa Karbala wakaelekea katika barabara inayo zunguka mji wa zamani kisha wakaingia katika barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s) halafu wakaingia katika malalo matukufu kisha wakatoka na kupita katika uwanja wa haram mbili tukufu na wakaishia katika malalo ya Kamanda wa Twafu mbeba bendera Abulfadhil Abbasi (a.s) wakiomboleza kumbukumbu ya kuzikwa miili mitukufu ya watu walio uwawa siku ya Ashura.

Riwaya zinasema kua siku ya tatu baada ya kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) kundi la wanawake wa kabila la bani Asadi walifika katika ardhi ya Twafu, wakaona maiti zimekatwa katwa na kuachwa bila kuzikwa zikiwa hazina vichwa katika mazingira yanayo Tisha yanayo onyesha ukubwa wa maafa katika historia ya mwanaadamu, bani Asadi wakabeba vifaa vya kuzikia na wakaenda eneo hilo kwa ajili ya mazishi, wakasimama wakiwa hawajui cha kufanya mbele ya maiti zile kwani hawajui huyu ni nani na yule ni nani, kwa sababu maiti zilikua hazina vichwa, wakiwa bado wanatafakari cha kufanya Imamu Zainul-Aabibina (a.s) akawafika eneo hilo, akajitambulisha kwao na akawaomba wamsaidie kuzika maiti zile, wakashirikiana naye na kuzika maiti hizo na huo ndio upekee wa kaabila hilo kihistoria, kwa ufupi hilo ndio tukio la msingi la chanzo cha uombolezaji wa bani Asadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: