Vituo vya Ashura: Mwezi kumi na tatu Muharam Imamu Sajjaad (a.s) azika mwili wa baba yake na watu wa nyumbani kwake pamoja na maswahaba zake watukufu…

Maoni katika picha
Wanahistoria wameandika kua bwana wa mashahidi (Sayyid Shuhadaa) (a.s), alifunga hema jangwani, na akawa anakusanya miili ya ndugu zake na maswahaba wake walio uwawa ndani ya hema kilo, kila shahidi (maiti) iliyo kuwa ikiletwa anasema (a.s): “Kifo (hiki) kinafanana na vifo vya Mitume na watu wa Mitume” ispokua ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) alimuacha palepale alipofia karibu na mto Furat.

Alipo ondoka Omari bun Saadi pamoja na familia ya Mtume (mateka) kwenda Kufa, aliwaacha wale ambao walisifiwa na kiongozi wa waumini (a.s) kuwa wao ndio mabwana wa mashahidi Duniani na Akhera katika jangwa wakipigwa na jua, akiwemo bwana wa vijana wa peponi, pamoja na kwamba walikua wanaangaziwa na nuru ya mbinguni, mwezi kumi na tatu Muharam akaja Zainul-Aabidina (a.s) kumzika baba yake (a.s), kwa sababu Imamu Maasumu hafanyiwi maziko ispokua na Imamu Maasumu kama yeye.

Hadari hizi zimedhibitishwa na majadiliano ya Imamu Ridha (a.s) pamoja na Ali bun Hamza, hakika Abulhassan Ridha (a.s) alimwambia: “Niambie kuhusu Hussein bun Ali, alikua ni Imamu? Akasema: Ndio, Ridha (a.s) akasema: “Nani aliye mzika?” Ibun Abi Hamza akasema: Alizikwa na Ali bun Hussein Sajjaad, Ridha (a.s) akasema: “Ali bun Hussein alikua wapi? Ibun Abi Hamza akajibu: Alikua mahabusu katika mji wa Kufa kwa Ibun Ziyadi lakini alitoka wao bila kujua akaenda kumzika baba yake kisha akarudi gerezani, Ridha (a.s) akasema: “Hakika aliye muwezesha Ali bun Hussein kuja Karbala kumzika baba yake kisha akaondoka, mwenye kufanya hivyo anaweza kuja Bagdad akamzika baba yake akiwa sio mahabusu wala mateka”.

Alipo fika Sajjaad (a.s) alikuta kundi la bani Asadi wametahayari hawajui wafanye nini, walikuwa wanashindwa kuzitambua maiti, kwani zilikua zimekatwa vichwa, wanaulizana hawa watu ni wakina nani na wanatoka katika familia zipi, akawaambia kuwa yeye ni nani na amekuja kuzika miili hiyo mitakatifu, akaanza kuwaambia majina yao na akawatambulisha bani Hashim miongoni mwao, wakapiga mayowe na kulia sana huku wanajipiga mashavuni kwao, Imamu Zainul-Aabidina (a.s) akaenda hadi kwenye mwili wa baba yake, akaukumbatia na akalia sana, akaenda sehemu ya kaburi akaondoa mchanga kidogo mara akaona kaburi tayali limesha chimbwa, akanyoosha mikono yake na kumshika chini ya mgongo wake akasema: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu na katika njia ya Mwenyezi Mungu na katika mila ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, amesema kweli Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Anacho taka Allah hakuna mwenye hila wala nguvu ispokua Allah mtukufu”, akamlaza kaburini pekeyake bila kusaidiwa na bani Asadi, akawaambia “Hakika ninao wanao nisaidia” baada ya kumlaza katika mwanandani, aliweka shavu lake katika shingo lake tukufu akasema: “Imefaulu ardhi inayo hifadhi mwili wako mtakasifu, hakika Dunia baada yako ni giza na Akhera inang’aa kwa nuru yako, hakika ni usiku wa giza na huzuni ya milele, au Mwenyezi Mungu awachagulie watu wa nyumba yako mji kama ambao wewe unaingia kuishi, nakutakia amani ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na rehma zake na baraka zake”, akaandika juu ya kaburi: “Hili ni kaburi la Hussein bun Ali bun Abu Twalib aliye uwawa ugenini akiwa na kiu”.

Kisha akaenda kwa ammi yake Abbasi (a.s) akamkuta akiwa katika hali ile ambayo iliwahuzunisha malaika wa mbinguni na wakalia Hurain wa peponi, akamkumbatia huku anasema: “Dunia ni chungu baada yako ewe mwezi wa bani Hashim, nakutakia amani ewe shahidi uliye faulu na rehma za Mwenyezi Mungu na baraka zake”, akamchimbia kaburi na kumzika peke yake kama alivyo fanya kwa baba yake, na akawaambia bani Asadi “Hakika ninao wanao nisaidia”.

Bani Asadi walishiriki kuwazika mashahidi, akawaonyesha sehemu mbili na akawaambia wachimbe makaburi, sehemu ya kwanza wakazikwa bani Hashim na sehemu nyingine wakazikwa maswahaba wa Imamu Hussein (a.s).

Aliye zikwa karibu zaidi na Imamu Hussein ni mwanaye Ali Akbaru (a.s), Imamu Swadiq (a.s) anasema kumuambia Hammaad Baswariy: “Abu Abdillahi aliuwawa akiwa mgeni, katika ardhi ya ugenini, analiliwa na aliye mzuri na anahuzunikiwa na hata ambaye hajamzuru, anaumizwa ambaye hajamshuhudia, anahurumiwa na kila anayeangalia kaburi la mtoto wake, walimwita kisha watu waovu wakamnyima haki na wakamfanyia vitimbi na kumuua na kumtelekeza aliwe na simba, walimzuia kunywa maji ya mto Furat ambayo hadi mbwa walikua wanayanywa, hawakumuheshimu Mtume (s.a.w.w) wala usia wake kwa watu wa nyumbani kwake, akaangukia katika njama zao pamoja na ndugu zake na wafuasi wake, akawa mpweke sehemu ya mbali na babu yake, mbali na nyumba ambayo haiheshimiwi ispokua na wale ambao wana imani ya kweli katika nyoyo zao na wanatambua haki zetu”.

Baba alinihadithia kua: Hakika tangu alipo uwawa sehemu ile haijakaa bila kuwepo wanaomtakia rehma miongoni mwa malaika au majini na binaadamu, na wote hao huwapongeza mazuwaru wake na humtakia kheri kila anaye angalia kaburi lake. Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu huwapongoza malaika kwa kumzuru. Na kinacho takiwa kwetu ni kumtakia rehma kila siku asubuhi na jioni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: