Kiwanda cha barafu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kiligawa kwa mawakibu Husseiniyya na mazuwaru zaidi ya vipande (elfu 20) vya barafu katika ziara ya Ashura…

Maoni katika picha
Ziara ya Ashura ya mwaka huu imeshuhudia ongezeko kubwa la joto, jambo lililo sababisha mawakibu zinazo hudumia watu pamoja na mazuwaru wahitajie zaidi barafu, kwa ajili ya kupozea maji wanayo gawa kwa mazuwaru au kwa ajili ya kuhifadhia chakula, ikabidi kiwanda cha barafu cha Atabatu Abbasiyya kiongeze uzalishaji wakati wa siku za ziara na baada ya siku hizo, kilifanikiwa kutengeneza zaidi ya vipande vya barafu (elfu 20) sawa na vipande (2,200) kila siku.

Wanufaika wa barafu hizo ni Mawakibu Husseiniyya na idara ya maji ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo inajukumu la kusambaza maji katika mahodhi yote yaliyopo ndani na nje ya haram tukufu, ikiwa ni pamoja na kugawa maji katika mawakibu zinazo toa huduma zilizo enea katika njia zote zinazo elekea kwenye malalo mawili matukufu, waliwapa vilevile kikosi cha wabiganaji cha Abbasi (a.s) shehena nyingine kwa ajili ya kugawia sekta zingine.

Kazi hii ilifanywa na magari maalumu ya utunzaji wa barafu ambayo yapo chini ya kiwanda, kiwanda kilifanya kila kiwezalo kuhakikisha kinakidhi mahitaji ya mazuwaru na mawakibu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: