Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zaomboleza kifo cha Sayyid Saajidina na Zainul-Aabidina Ali bun Hussein (a.s)…

Maoni katika picha
Huyu ndiye mji wazijua nyayo zake ** na nyumba yamtambua na hillu na haram.

Huyu ni mtoto wa mja mwema kuliko wote ** huyu ni mchamungu msafi mtakasifu.

Huyu ni mtoto wa Fatuma kama ulikua humjui **

babu yake ndiye hitimisho la mitume wa Allah.

Wamejaza wema kwa walimwengu na sasa unatoweka ** wema unapotea na kutoweka.

Makuraishi wakimuona husema msemaji ** ukarimu wa huyu ndio kilele cha ukarimu.

Anainama kwa haya na anamvulilia anaye muudhi ** haongei ispokua akiwa anatabasamu.

Ni Sajjaad Pambo la waabudio na bwana wao mtu aliyekua na sugu katika viungo vya sajda kutokana na wingi wa ibada, kiongozi wa waumini na mbora wa watu wanaomsujudia Mwenyezi Mungu mtukufu, yeye ndiye kumbukumbu ya Twafu na mzikaji wa miili mitukufu, na ndio safina ya uongofu na mti wa elimu tunao faidika na kivuli chake, ni Imamu Ali bun Hussein (a.s).

Kutokana na kumbukumbu ya kifo chake, katika uwanja wa haram tukufu ya Abbasi kumewekwa kitambaa kinacho ashiria huzuni maalumu kwa kifo chake (a.s), na kimeandikwa maneno ya utii na huzuni kutokana na misiba iliyo tokea katika mwezi huu, wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) wanaendeleza huzuni zao na kutoa pole kwa Imamu Mahdi (a.f) katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kila mtu anajua ukubwa wa msiba huu na namna unavyo umiza nyoyo za waumini, kutokana na matatizo aliyo pata Imamu wao wa nne, aliye chukuliwa mateka na akashuhudia chuki za bani Umayya Dunia ikabadilika, akaja kuuwawa kishahidi kwa kupewa sumu akiwa ni mwenye kufanya subira na kumtegemea Mola wake, kutokana na mambo waliyo fanyiwa nyoyo za waumini hubaki na huzuni kipindi cha mwaka mzima na huongezeka zaidi katika mwezi wa Muharam.

Baada ya swala za Duhuraini katika siku ya Alkhamisi (24 Muharam 1440h) sawa na (4 Oktoba 2018m), kwa unyenyekevu na huzuni kubwa huku wakiimba kaswida zinazo amsha hisia za huzuni, watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya matembezi ya kuomboleza na kutoa pole kwa Imamu Hujjat Almuntadhir (a.f) na kwa Imamu Hussein kutokana na kifo cha Imamu wa nne, Imamu Zainul-Aabidina na Sayyidu Saajidina Ali bun Hussein (a.s).

Matembezi hayo yalianzia katika uwanja wa haram ya mnyweshaji wenye kiu na mbeba bendera Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapitia katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, wakati wanatembea waliendelea kuimba kaswida zinazo amsha hisia za huzuni kutokana na msiba huu mkubwa, walipo wasili katika malalo ya bwana wa vijana wa peponi Imamu Hussein (a.s), walipokelewa na ndugu zao watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu, wakaendelea kuimba kaswida za kuomboleza kisha wakafanya majlisi ambayo walizungumzia msiba huu na dhulma alizo fanyiwa Sayyid Saajidina Imamu Ali bun Hussein (a.s).

Imamu Sajjaad ni Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s), ni Imamu wa nne katika Maimamu wa Ahlulbait (a.s), jina lake la kuniya huitwa Abulhassan, na majina ya laqabu (sifa) mashururi zaidi ni Zainul-Aabidina na Sajjaad, alizaliwa katika mji wa Madina mwaka wa (38h), aliishi na babu yake Amirul Mu-uminina (a.s) kwa miaka miwili, na akaishi na ammi yake Imamu Hassan (a.s) miaka kumi, na akaishi na baba yake Imamu Hussein (a.s) miaka ishirini na moja, baada ya kifo cha baba yake akaishi miaka thelathini na nne, alifia katika mji wa Madina kwa kupewa sumu mwaka wa (95h), akiwa na miaka hamsini na saba, alichukua ramsi madaraka ya Uimamu baada ya kifo cha Imamu Hussein (a.s) katika vita ya Twafu, ambayo aliuwawa yeye pamoja na watu wa nyumbani kwake (a.s), alishuhudia mauwaji waliyo fanyiwa Ahlulbait (a.s) katika ardhi ya Karbala, amani iwe juu ya Hussein na Ali bun Hussein na watoto wa Hussein na maswahaba wa Hussein.

Tunapenda kukumbusha kua Atabatu Abbasiyya tukufu kama kawaida yake katika kila tukio la aina hii, imeandaa ratiba ya kuomboleza yenye vipengele tofauti, kuna utowaji wa mihadhara ya dini, na kufanya majlisi za kuomboleza, pia mawakibu za Karbala zinajiandaa kufanya matembezi ya kuomboleza mwezi (25) Muharam, ambapo watakuja kumpa pole Sayyid Shuhadaa kwa kifo cha mtoto wake Sajjaad (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: