Mawakibu Husseiniyya zamiminika katika mji mtukufu wa Karbala kwenye malalo mawili matukufu kuomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s)…

Maoni katika picha
Ilipo chomoza asubuhi ya Alkhamisi mwezi ishirini na tano Muharam, Mawakibu Husseiniyya zimeanza kumiminika katika mji mtukufu wa Karbala, na kuelekea katika malalo mawili matukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuomboleza kifo cha Imamu Ali bun Hussein Zainul Aabidina (a.s).

Kama kawaida matembezi ya mawakibu yalianzia katikati ya mji, wakiwa wamebeba bendera huku wakiimba kaswida zinazo amsha hisia za huzuni na kuelekea katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) kumpa pole yeye pamoja na Hujjat bun Hassan (a.f), kutokana na msiba huu mkubwa, kisha baada ya hapo wanatoka na kuelekea katika malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, huku wakilia kwa majonzi kutokana na yaliyo tokea katika ardhi ya Twafu, miongoni mwa mambo ambayo hutia simanzi na majonzi katika nyoyo za wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s), mawakibu hizo zinapo wasili katika uwanja wa haram tukufu ya bwana wa mashahidi (a.s), zinafanya majlisi ya kuomboleza na kupiga matam sambamba na kumpa pole mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) kutokana na msiba huu.

Kwa upande wake uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, pia kutokana na ratiba yake ya kuomboleza katika mwezi huu wa Muharam na kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Imamu Zainul Aabidina (a.s), umefanya majlisi maalumu kwa watumishi wa Ataba tukufu kwa ajili ya kuomboleza msiba ulio ukumba umma wa kiislamu wa kifo cha Sayyid Saajidina mgonjwa wa Karbala na mzikaji wa miili mitakatifu.

Majlisi ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha akapanda kwenye mimbari Sayyid Adnani Mussawi na akatoa muhadhara unaohusu utukufu wa Imamu Sajjaad (a.s) na nafasi yake muhimu katika kuelezea tukio la Twafu, akabainisha kua kama sio yeye Twafu isinge tajwa, hali kadhalika alizungumzia upande wa tabia zake tukufu (a.s), zilizo asisi kwa shia (wafuasi) wake mwenendo bora wa tabia na ubinadamu ambao hauta potea hadi siku ya kiyama, akahitimisha muhadhara wake kwa kusoma kaswida ya huzuni yenye beti zinazo elezea dhulma alizo fanyiwa Imamu Ali bun Hussein Sajjaad (a.s) na namna alivyo uwawa kwa sumu iliyotoka kwa kiumbe muovu zaidi.

Kumbuka kua Mawakibu Husseiniyya hazija acha kumiminika katika mji mtukufu wa Karbala tangu siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam na zitaendelea hadi mwisho wa mwezi, kisha zitajiandaa kuwapokea na kuwahudumia mazuwaru wa ziara ya Arubaini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: