Usia na maelekezo ishirini yaliyo tolewa na Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Ayatullahi Sayyid Sistani kwa wapiganaji wa fatwa tukufu ya kujilinda, umepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wahudhuriaji wa kongamano linalo simamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika jengo la umoja wa mataifa, nakala ya usia na maelekezo hayo ilitafsiriwa na Atabatu Abbasiyya na kuandikwa katika umbo la kijitabu kilicho kusanya usio na maelekezo yote yaliyo wapa nguvu wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa Hashdi Sha’abi, waliyafanyia kazi maelekezo hayo na ikawa ni sababu ya kuwashinda magaidi wa Daesh.
Kwa kua kongamano limehudhuriwa na watu wa Dini tofauti, ilikua ni fursa nzuri ya kuutambulisha usia huo kupitia machapisho yake hayo, kwani asilimia kubwa ya wahudhuriaji walikua hawajapata nakala halisi ya usia na maelekezo hayo, na baadhi yao waliusikia katika vyombo vya habari ambavyo viliuelezea kimakosa, na vingine viliupotosha kwa lengo la kupoteza ukweli, wahudhuriaji wengi wamekiri kua usia huu na maelekezo haya ni sawa na muhtasari wa kanuni za umoja wa mataifa katika maswala ya aina hii (ya kivita).
Dokta Maitham Radhawi ambaye ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano hili na mwakilishi wa taasisi ya Imamu Khui katika umoja wa mataifa amesema kua: “Kwa ujumla kongamano limepata mafanikio makubwa, mafanikio haya yametokana na mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo, ni kitendo kilicho fanywa na ujumbe wa Atabatu Abbasiyya cha kugawa usia na maelekezo ya Ayatullahi Sayyid Sistani aliyo wapa wapiganaji walio itikia wito wa kulinda taifa lao na maeneo matukufu, usia ulio wapa nguvu wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa kujitolea walio itikia wito wa fatwa tukufu ya kujilinda na wakafanikiwa kuwashinda magaidi wa Daesh. Hakika usia huu umeathiri sana nyoyo za wahudhuriaji wa kongamano hili, kuna walio acha kusikiliza maelezo yanayo endelea katika kongamano na wakawa wanasoma na kutafakari usia huu na maenelezo ambayo yameuonyesha ulimwengu utukufu wa uislamu, maelekezo hayo yamesisitiza umuhimu wa kumuokoa dhaifu na kumsaidia mnyonge anaye stahiki msaada, kama ilivyo katika historia ya Mtume (s.a.w.w), pia yameasisi uwelewa wa maana ya ushindi na kushinda”.