Kituo cha Imamu Ridha (a.s) katika jimbo la Kotagen nchini Ujerumani chafanya nadwa ya wazi kwa ajili ya kusherehekea ujio wa ugeni kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Maoni katika picha
Kituo cha Imamu Ridha (a.s) kimefanya nadwa ya wazi kwa ajili ya kusherehekea ujio wa wageni kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hafla ya nadwa hiyo imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu walio tangulia mbele ya haki, halafu ukaimbwa wimbo wa Ibaa.

Katika nadwa hiyo uliwasilishwa ujumbe mbalimbali ukitanguliwa na ujumbe wa wageni walio kuja kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ulio wasilishwa na Sayyid Muhammad Ali Bahrul-Uluum, kundi kubwa la waislamu ambao ni wahamiaji wanao ishi katika mji wa Kotagen wameshiriki katika nadwa hiyo pamoja na wawakilishi wa baadhi ya vituo vya kiislamu kutoka miji tofauti.

Ujumbe wa Sayyid Muhammad Ali Bahrul-Uluum ulijikita katika kuelezea umuhimu wa kushikamana na mwenendo wa Ahlulbait (a.s) na kuwafuata, pamoja na kua mabalozi wa fikra za Ahlulbait (a.s) kwani wao ni mfano mwema katika jamii.

Pia ilihudhuriwa na idadi kubwa ya wasomi wa sekula na waandishi wa habari, ugeni ukatoa zawadi kwa kituo hicho kutokana na kukamilika kazi ya ujenzi kwenye kituo hicho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: