Katika kongamano lililofanyika kwenye jengo la umoja wa mataifa huko New York: viongozi wakubwa wajitokeza kupiga picha!! Kwa sababu...

Maoni katika picha
Kongamano la kimataifa la kwanza (Kurudisha heshima ya elimu kwa ajili ya kuupa nguvu uadilifu wa kijamii), lililo ratibiwa na uongozi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa kushirikiana na taasisi ya Imamu Khui pamoja na umoja wa tafiti za kielimu na turathi na kufanyika ndani ya jengo la umoja wa mataifa, kongamano hilo lilikua na matukio mbalimbali, yapo matukio yaliyo pangwa katika ratiba na yapo yaliyo zuka ghafla.

Miongoni mwa matukio hayo ni tukio la kupandisha bendera ya kubba la Imamu Hussein pamoja na ya kubba la Mbeba bendera wake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ukumbi wa uchumi ndani ya jengo la umoja wa mataifa katika jimbo la New York Marekani ambao ndio ukumbi ulio tumika kuendeshea kongamano hilo.

Halikufungwa pazia la kongamano hadi baada ya kukunjuliwa bendera za kubba tukufu jukwaani huku zikipigwa swalawatu kwa wingi na wengine wakisema: (Labbaika yaa Hussein), wahudhuriaji wakajitokeza kwa wingi kufanya tabaruku na kupiga bicha huku wahudumu wa ukumbi wakiangalia kwa mshangao tukio hilo.

Mtandao wa kimataifa Alkafeel ulikuwepo katika tukio hilo, lililo pelekea hadi baadhi ya washiriki kusukumana.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano na mwakilishi wa taasisi ya Imamu Khui Dokta Maitham Radhawi amebainisha kua: “Kusukumana huko kunaonyesha namna wanavyo mpenda Imamu Hussein (a.s), ukizingatia kua tupo katika siku za kukumbuka kifo chake na kutekwa familia yake, hivyo vitendo vyao havikutokana na matashi yao wala hisia zao, ilikua kama vile baada ya kuona bendera zimewavuta na kuwaunganisha nae kwa nguvu ya ajabu”.

Dokta Shaukat Asghari akaongeza kua: “Hakika ni jambo la kawaida kuona watu wakizipupia bendera hizi ambazo zina nafasi kubwa katika nyoyo za waislamu wote, Imamu Hussein (a.s) anapendwa na kila mtu bila kujali tofauti za mitazamo na madhehebu au viwango vya elimu, mambo yote yamefanyika kutokana na mapenzi ya dhati juu yake”.

Naye Mushtaqu Abbasi Muan ambaye ni miongoni mwa wajumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu akasema kua: “Hakika kupupiwa bendera hizi kunamaanisha ujumbe wa amani walionao wapenzi wa Imamu Hussein (a.s) kwa kila mtu huru Duniani, wanathibitisha kua wanafuata mwenendo wake wa islahi alio uandika kwa damu yake takatifu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: