Kutoka Basra hadi Karbala kwa mwaka wa pili mfululizo kituo cha uandaaji wa vipindi Alkafeel chaandaa masafa ya bure itakayo tumika kurusha matembezi ya wapenzi wa Hussein kwa ubora wa mkubwa…

Maoni katika picha
Mwaka wa pili mfululizo kituo cha uandaaji wa vipindi Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni kimeandaa masafa maalumu kwa ajili ya kurusha bure matembezi ya wapenzi wa Hussein kuanzia mbali kabisa kusini mwa Iraq hadi katika Kaaba ya msimamo Karbala tukufu, kwa kutumia vifaa vya kisasa chini ya watu walio bobea katika fani hiyo, wanatumia kila njia kufikisha sauti ya ziara hii kila sehemu ya Dunia.

Wametoa wito kwa vyombo vyote vya habari vya kitaifa na kimataifa vitakavyo penda kurusha matangazo hayo wanaweza kutumia anuani zifuatazo:

E3B at 3.1 °E

Down:11595.9 H

SR:2500

DVBS2

8PSK

FEC:3/4

HD/MPEH-4
matangazo hayo yatarushwa kwa ratiba ifuatayo:

  • 1- Saa 02:00 asubuhi hadi saa 05:30 asubuhi watembea kwa miguu.
  • 2- Saa 05:30 asubuhi kisomo cha Qur’ani tukufu na swala ya Adhuhuri na Alasiri kutoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu.
  • 3- Saa 09:00 jioni hadi saa 11:30 jioni watembea kwa miguu.
  • 4- Saa 11:30 kisomo cha Qur’ani tukufu na swala ya Magharibi na Isha kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • 5- Siku ya Juma Nne na Alkhamisi kutakua na kipindi maalumu cha kiibada kitakacho fanywa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu saa 08:00 Adhuhuri.
  • 6- Iwapo yakitokea mabadiliko yeyote yatatangazwa siku moja kabla InshaAllah.

Fahamu kua matangazo hayo yatafanyika saa 24.

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba:

09647732407567 / Muhandisi wa urushaji wa vipindi. Na: 09647706007187 / Idara ya kituo.

Chombo cha habari kitakacho shindwa kufuatilia matangazo yetu kwa kutumia anuani tulizo taja, kinaweza kufuatilia kupitia mitandao ya kijamii, (Facebook) katika ukurasa ufuatao:

https://www.facebook.com/alkafeel.for.artistic.production/
Au katika ukurasa ya Youtube ufuatao:

https://www.youtube.com/channel/UCy0MMgRho_O8jxiIj46qMxw
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: