Shekh Hussein Turabi ambaye ni mkuu wa Maahadi hiyo ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika kazi hii ni sehemu ndogo ya kazi nyingi zilizo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta mbalimbali, na tumeanza kuweka ndoo hizi ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi katika njia zinazo tumiwa zaidi na mazuwaru, vilevile Maahadi imechukua jukumu la kufanya usafi katika baadhi ya maeneo sambamba na kusambaza ndoo za kuwekea taka.
Akaongeza kua: “Ndoo za kuwekea taka zenye ukubwa tofauti zimewekwa katika nguzo za taa zilizopo katikati ya barabara, na zimeandikwa ujumbe unao himiza kutunza usafi, tumesambaza sehemu tatu, ambazo ni:
- 1- Barabara ya (Bagdad – Karbala).
- 2- Barabara ya (Baabil – Karbala).
- 3- Barabara ya (Najafu – Karbala).