Baada ya kufanya maboresho na kuongeza kamera za kisasa: Atabatu Abbasiyya tukufu yawasha mtambo wa kamera ya kuhesabu mazuwaru…

Maoni katika picha
Jopo la mafundi na wahandisi wa idara ya mawasiliano ya Atabatu Abbasiyya tukufu imewasha mtambo wake mkuu wa kuhesabu watu wanaokuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika msimu wa Arubaini, baada ya kuongeza program mpya na kamera za kisasa zenye uwezo mkubwa wa kutunza idadi ya mazuwaru.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara Muhandisi Farasi Abbasi Hamza, ambaye amesema kua: “Baada ya mafanikio yaliyo patikana miaka ya nyuma ya kutoa idadi sahihi ya mazuwaru tena kwa umakini na hesabu inayo endana na uhalisia, mwaka huu tumeboresha zaidi na kufunga kamera pande kuu zote zinazo ingia Karbala, ambazo ni upande wa Najafu, Hilla, Bagdad na upande wa Husseiniyya pamoja na upande wa Huru, ambazo ndio njia zinazo tumiwa na asilimia kubwa ya mazuwaru”.

Akabainisha kua: “Hakika upanuzi huu umehusisha ufungaji wa kamera za ziada katika maeneo yaliyo fungwa kamera mwaka jana pamoja na maeneo mapya taliyo ongezwa mwaka huu, jumla tumefunga kamera sehemu tano wakati mwaka jana tulifunga sehemu nne, kila sehemu imeonganishwa na mtambo mkuu wa kuhesabu watu uliopo katika chumba cha kusimamia uhesabuji (Control room) kilichopo Atabatu Abbasiyya tukufu, na mtambo huo ni wa kisasa zaidi, kupitia mtambo huo tutakusanya taarifa za kila siku na kuzitunza katika ripoti, halafu tutafanya majumuisho na kuyatangaza mwishoni mwa ziara, kama tulivyo kua tukifanya miaka ya nyuma”.

Pia Muhandisi Farasi amesema kua: “Wamefunga mtambo maalumu unao hesabu watu wanao ingia na kutoka ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: