Kitengo cha Dini kimeanza kutekeleza mradi maalumu ya tablighi kwa mazuwaru wa Arubaini…

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kutekeleza mradi maalumu wa tablighi kwa mazuwaru wa Arubaini wanaokuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kimeandaa idadi kubwa ya Mashekhe na Masayyid wanao fanya kazi katika kitengo hicho pamoja na wale wa kujitolea, na kuwaweka katika vituo vyake kilivyo viweka kwenye barabara zinazo ingia Karbala tukufu, vituo ambavyo vipo ndani ya mradi maalumu wa tablighi kwa mazuwaru wa Arubaini ambao unasimamiwa na hauza ya Najafu Ashrafu na kwa baraka ya Marjaa Dini mkuu.

Vituo vya tablighi vipo katika barabara kuu zinazo ingia Karbala ambazo ni; barabara ya Najafu, Baabil na Bagdad, kwenye majengo yanayo hudumia mazuwaru yaliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu au katika baadhi ya mawakibu zenye watu wengi.

Vituo hivi vya tablighi vinatoa huduma ya kujibu maswali ya kidini yanayo husu Fiqhi, Aqida na mengineyo, pia mubalighina wa vituo hivyo wanaongoza swala za jamaa katika sehemu walizopo, pamoja na kugawa vipeperushi vyenye mafundisho ya Dini na machapisho maalumu ya ziara ya Arubaini, na wanatoa nasaha kwa mazuwaru kwa kutumia vipaza sauti, sambamba na kutoa mihadhara kuhusu mafundisho ya ziara na mambo mbalimbali siku nzuma.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: