Hawa hapa wapenzi wa Imamu Hussein (a.s) wanaendelea kumiminika katika mji wa Karbala tukufu kuhuisha utiifu wao kwa Abu Abdillahi Hussein (a.s), misafara ya mazuwaru watembea kwa miguu ilianza kuondoka katika wilaya ya Ramitha kwa kutumia barabara kuu pamoja na barabara ndogo hadi katika mkoa wa Diwaniyya kisha katika mkoa wa Hilla kupitia wilaya ya Qassim, na wengine wanapitia katika mkoa wa Najafu halaru wanakwenda hadi Karbala.
Mwandishi wa mtandao wa kimataifa Alkafeel anaripoti kua: “Mkoa wa Diwaniyya umepokea makundi mengi ya mazuwaru, na haukufanya ajizi katika kuwahudumia kwenye njia zote walizo tumia, kupitia mawakibu na vikundi vya Husseiniyya au idara za serikali, na wote kwa ujumla wamefanya kila wawezalo katika kutoa huduma”.
Mikoa mingine kama vile Waasit na Misaan bado misafara ya mazuwaru inaendelea kumiminika, misafara yote inakutana katika mkoa wa Baabil kisha ndio inaelekea Karbala. Kamera ya mtandao wa Alkafeel imeshuhudia matembezi hayo na unakuletea baadhi ya picha zake.