Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chatoa agizo la utunzaji wa majingira na mali za umma…

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimetoa agizo kwa wahudumu wa mawakibu wahakikishe wanatunza mazingira na mali za umma, wasiharibu miti iliyo pandwa pembezoni mwa barabara na katika mabustani na maeneo ya wazi wakati wanapo toa huduma, kwa sababu jambo hili linapingana na misingi ya kisheria na linaharibu thawabu za kazi hiyo tukufu, kama koso hilo likithibitika kufanywa na maukibu yeyote itakua ni sababu ya kuzuiliwa kushiriki katika ziara zijazo, tunaomba wapewe nafasi wahudumu wa miti hiyo watakapo hitaji kumwagilia na kuichambulia au kufanya kazi yeyote katika miti hiyo.

Kuna baadhi ya mawakibu zimejenga mabanda ya kutoa huduma sehemu zinazo funga njia, na wengine wamefanya uharibifu katika miti hiyo ambayo kwa asilimia kubwa imepandwa katika mradi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, mradi wa upandaji wa miti katika mkoa wa Karbala tukufu, ambapo zimetumika pesa nyingi na nguvu kubwa, tayari sasa hivi miti hiyo imebadilisha picha ya muonekano wa mji, pamoja na kua maukibu zinatoa huduma muhimu lakini hazitakiwi kuharibu miti tena ambayo ni wakfu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kila mti umewekewa alama ya utambulisho.

Kumbuka kua kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimesha toa maelekezo maalumu katika ziara ya Ashura ya Imamu Hussein (a.s), ikiwa ni pamoja na kuhimiza utunzaji wa mazingira na utunzaji wa miti iliyopo pembezoni mwa barabara zinazo elekea katika haram mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: