Idara ya kunufaika na mitambo ya Atabatu Abbasiyya tukufu yatangaza huduma inazotoa katika ziara ya Arubaini…

Maoni katika picha
Idara ya kunufaika na mitambo ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza shughuli zake katika ziara ya Arubaini, ambazo zina vipengele vingi kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wake Sayyid Mustafa Dhiyaau-Dini, kama ifuatavyo:

  • 1- Kuandaa magari kwa ajili ya kupokea wageni wanaokuja kutoka nje ya nchi na kuwaandalia ratiba maalumu ya kuwapeleka katika Ataba zote na mazaru tukufu za hapa Iraq kuanzia (9 Safar) hadi (25 Safar) pamoja na kuwarudisha katika viwanja vya ndege baada ya kulamiza ziara.
  • 2- Kupokea mazuwaru katika viwanja vya ndege na maeneo ya mipakani katika kipindi chote cha ziara.
  • 3- Kuratibu uingiaji na utokaji wa gari za Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya mji wa Karbala katika kipindi cha ziara ya Arubainiyya.
  • 4- Kuandaa gari za kuwapeleka mubalighina na mubalighati katika mawakibu (vituo) vyao vilivyopo katika njia ya pepo (barabara ya Baabil, Najafu na Bagdad) kwenda kutekeleza majukumu yao ya kitablighi.
  • 5- Kutoa huduma kwa mawakibu zilizo sambaa katika barabara zote zinazo elekea Karbala, kama vile kubeba mabeji na mahitaji ya lazima kwa mazuwaru pamoja na vyakula kwa kutumia gari za mizigo na kwa nyakati tofauti.
  • 6- Kuandaa gari za aina tofauti kwa ajili ya kuwachukua na kuwapeleka mazuwaru katika malalo na mazaru zote.
  • 7- Kuvipa gari maalumu baadhi ya vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kama vile kitengo cha mahusiano kwa ajili ya kupokea wageni wanaokuja Karbala kila siku.
  • 8- Idadi ya mazuwaru inaongezeka kila siku, pamoja na kwamba sisi tunazingatia muda na tarehe na tumeweka utaratibu mzuri, tumeandaa tiketi zinazo fanana na tiketi za ndege, zina jina la dereva, namba yake ya simu, jina la mhudumiwa, namba yake ya simu pamoja na anuani yake na tarehe na muda wa safari yake.

Dhiyaau-Dini akabainisha kua: “Kuna ufuatiliaji wa utendaji wa gari zote zilizo chini ya idara hii, kwa kufuata ratiba maalumu ambayo huchapishwa kila siku na kupewa watumishi wa idara, ratiba huonyesha kazi zitakazo fanywa na gari katika siku hiyo ndani na nje ya mkoa wa Karbala, kazi zote huingizwa katika shughuli za siku zinazo fanywa na idara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: